Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa Wabunge wawili kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania.

 

Kwanza Rais Magufuli amemteua Humphrey Polepole kuwa Mbunge Katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Polepole ni Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM – NEC, itikadi na uenezi.

 

Taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Rais Magufuli pia amemteau Riziki Lulida kuwa Mbunge Katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bi Lulida alikua pia Mbunge wa viti maalumu Katika Bunge la 11.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Wabunge wateule wataapishwa Kwa mujibu wa sheria za taratibu za Bunge.