Wakulima 43 wa Jimbo la Borno, Nchini #Nigeria wamechinjwa katika mashamba ya mpunga yaliyopo Zabarmari na Kikundi cha Boko Haram


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kupitia Ukurasa wake wa Twitter ameonesha kusikitishwa na kitendo hicho, pia amelaani mauaji hayo. Amesema kuwa, Serikali ya Nigeria imefanya yote yanayowezekana kulinda nchi hiyo na watu wake.


Aidha, Shirika la Kimataifa Linalohusika na Haki za Binaadamu, Amnesty International limelaani kitendo hicho