MGOMBEA Urais wa Marekani kupitia Chama Cha Democratic, Joe Biden ameshinda uchaguzi wa Marekani na kuwa rais mteule wa Marekani baada ya kumshinda mgombea urais kupitia Chama Cha Republican ambaye pia alikuwa akitetea kiti chake, Donald Trump.

Biden ameshinda katika jimbo muhimu la Pennsylvania (kura 20) na Nevada (kura 6|), akijizolea kura zaidi ya 270 zilizohitajika ili kunyakua kiti cha White House baada ya kupata kura 290 huku Trump akisalia na kura 214 mpaka sasa


Aidha, Kampeni ya Trump imeonesha mgombea wao hana mpango wa kukubali matokeo ya uchaguzi huo. Matokeo hayo yanamfanya Trump kuwa rais wa kwanza kutumikia awamu moja madarakani tangu miaka ya 1990.

Majimbo mawili ya North Carolina ambalo anaongoza Trump kwa kura nyingi na Georgia ambalo anaongoza Biden kwa kura nyingi bado hayajatangazwa mpaka sasa.