Arsenal, Chelsea na Tottenham zinamtaka beki wa Bayern Munich Jerome Boateng. Mjerumani huyo aliye na umri wa miaka, 32, huenda akaondoka kwa uhamisho wa bila malipo baada ya Bayern kuonesha ishara kwamba haina mpango wa kumpatia mkataba mpya. (Bild, Sun)
Wolves wameanza kukwazika na winga wao Adama Traore, ambaye hajatia saini mkataba mpya. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 24, wiki iliyopita alikubali mkataba mpya kwa masharti lakini hajajitolea kuutekeleza. (90min)
Chelsea inatarajiwa kuwasilisha dau lingine la kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice mwezi Januari. The Blues watawauza wachezaji wawili wakubwa kufadhili uhamisho wa Declan Rise aliye na miaka 28. (Football Insider)
Liverpool wanatafakari uwezekano wa kumnunua mlinzi wa zamani wa Uholanzi na Watford Daryl Janmaat, 31, kama hatua ya muda mfupi ya kuimarisha safu yake ya ulinzi inayokabiliwa na changamoto. (Teamtalk)
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England pia wanamnyatia beki wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 22, ambaye yuko kwenye orodha ya kuimarisha zaidi safu yao ya ulinzi. (The Athletic – subscription required)
Arsenal wamepata wamepata matumaini mapya katika jaribio lao la kumsajili kiungo wa kati wa RB Salzburg Dominik Szoboszlai, 20, baada ya ajenti wa mchezaji huyo raia wa Hungary kukanusha madai kwamba anahamia RB Leipzig. (Mirror)
Hatma ya mkufunzi wa West Brom Slaven Bilic haijulikani- huku klabu hiyo ikiendelea kuandikisha matokeo mabaya katika Ligi ya Premia msimu huu – tetesi zinaarifu kuwa Lee Bowyer wa Charlton ni miongoni mwa majina yanayopigiwa upatu kuchukua nafasi yake. (Mirror)
Kiungo wa kati wa zamani wa Denmark na Tottenham Christian Eriksen, 28, anasema hali lake ya sasa “haikua ndoto yake”. (TV2, via Goal)
Real Madrid inatarajiwa kuwapunguzia tena marupurupu wachezaji wake kutokana na athari za janga la virus vya corona. (ESPN)
The post Arsenal, Chelsea na Tottenham katika vita nzito dhidi ya nyota wa Bayern Munich appeared first on Bongo5.com.