Baba Mlezi wa msanii wa muziki Diamond Platnumz, @uncle_shamte ameamua kutoa la moyoni juu ya baadhi ya watu kuongelea mahusiano ya watu pasipo kujua nini hasa kipo kati yao.


Uncle Shamte amefunguka hayo kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuandika

“Si vyema sana kuongelea mahusiano ya watu hadharani au kwa lugha nyingine hayatuhusu, lakini jamii inapaswa kuamini kuwa... KUNA KITU KIKUBWA SANA MUNGU AMEKIPANGA KWA WATU WAWILI HAWA NA VYEMA TUMUACHIE YEYE MUNGUAAMUE!#WekaUtimuPembeniAngaliaNguvuYaMuunganoWaoNiAlamaYaUpendoTu.”

Maneno hayo yaliendana na picha iliyowekwa akimuonesha Diamond na Zari. Habari Za Chini Chini, Inaelezwa Diamond Atamuoa Zari, Ambaye Ni Mzazi Mwenzie Wa Watoto Wawili ( @princess_tiffah × @princenillan )