KUMEKUCHA tena! Kama ulikuwa unajiuliza kuhusu kubuma kwa ndoa ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’; usipate shida sana, miongoni mwa sababu ambazo zimetajwa kuwa kizingiti cha ndoa hiyo ni pamoja na jamii ya siri ya Freemason, IJUMAA WIKIENDA linakupa mchapo kamili.


 


Ndoa ya mkali huyo wa Bongo Fleva na Bosi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond au Mondi ilitarajiwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu, lakini siku hiyo ikapita kimyakimya kama vile hakuwahi kutangaza kabla.


 


FREEMASON WATAJWA


Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kimeeleza kuwa, siri iliyopo nyuma ya pazia ya Mondi kutooa ni kutokana na yeye kuhusishwa na jamii hiyo ya siri (secret society) ya Freemason inayohusishwa na imani za kishetani.


 


“Freemason ndiyo huwa hawapendagi kabisa mtu wao aoe, huwa wanapenda awe peke yake tu na ikitokea mhusika akalazimisha kuoa, basi linaweza kutokea jambo baya,” kilisema chanzo hicho.


 


DATA ZASHUSHWA


Chanzo hicho, mbali na kulieleza Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, kilitoa vyanzo mbalimbali vya mitandao ya kijamii ambavyo vilionesha jinsi Mondi anavyozuiwa kuoa na jamii hiyo ambayo ina ukaribu mkubwa mno na tasnia ya muziki na sanaa kwa jumla duniani.


 


“Mitandao mingi tu ilishajadili sana suala hili. Mingi ilieleza kwa kirefu ni namna gani kutakuwa na ugumu sana kwa Mondi kuoa kama kweli ana ushirikika na jamii ya Freemason,” kilisema chanzo hicho.


 


IJUMAA WIKIENDA LAPERUZI


Gazeti hili la IJUMAA WIKIENDA liliperuzi mitandao hiyo ambayo mingi ilikuwa haina ushahidi wa moja kwa moja kama kweli Mondi anashirikiana na jamii hiyo, lakini zaidi walijadili jinsi gani kuna ugumu kuoa ukiwa ndani ya jamii hiyo.


 


“Unajua kuna kama viapo huwa unakula kabla ya kuingia Freemason sasa kama yeye alikubali kuwa anahitaji utajiri na akakubali hataooa zaidi ya kuzaa ni ngumu sana sasa hivi kuoa, mtakuwa mnasikia tu anatangaza halafu kimya,” kilisema chanzo hicho na kumalizia.


 


“Nasikia mama Mondi huko sasa hivi anakosa la kusema na kubaki mdomo wazi maana yeye anataka ndoa, lakini mwanaye hawezi kukubali.”


 


MENEJA AFUNGUKA


Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilifanya jitihada za kumtafuta mmoja wa mameneja wa Mondi, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ ambapo alifunguka kuwa mambo bado kwani kampeni za uchaguzi zimeingilia kati ndiyo sababu ndoa ya Mondi ambapo meneja huyom amekanusha kuwa si kweli maana wao hawapo vikao vitaendelea vipi?


 


“Kuhusu vikao…vitaendelea vipi wakati sisi sote hatupo, kiukweli bado na kitu cha msingi ni kwamba, sina uwezo wa kuzungumza lolote maana sina jipya na mimi sipendi kuwaongopea wananchi,’’ alisema Mkubwa Fella.


 


ALICHOSEMA MAMA MONDI…


Katika siku ya kuzaliwa ya Mondi ya Oktoba 2, mwaka huu, akitimiza umri wa miaka 31, mama mzazi wa staa huyo, Sanura Kassim ‘Sandra’ au ‘Mama Dangote’, alifunguka kwenye moja ya mahojiano na chombo cha habari kuwa, anamtakia umri mrefu mwanaye na aoe kabla yeye hajafa.


 


“Najisikia furaha na faraja maana hata mimi naona nimekua, kama leo (Ijumaa iliyopita) hivi Nasibu (Mondi) kaongeza umri na ametimiza miaka thelathini (ameghafi lika ni miaka thelathini na hakuna kitu kipya.


 


“Kwa kipindi sijaongea naye (Mondi), siwezi kuzungumza chochote kwa sababu niko kwenye kampeni na yeye yuko kwenye kampeni za mheshimiwa Rais Magufuli. “Nadhani likimalizika hili, tutakaa chini ili tujue tunafanyaje na nitakuwa na jibu zuri,” anasema Mkubwa Fella.


 


VIKAO VYA CHINICHINI


Habari zilisambaa kuwa vikao vya chinichini vinaendelea kuhusiana na moja), nafurahi sana. “Mimi kila siku ya kuzaliwa ya mwanangu huwa namtakia umri mrefu, aishi na watu vizuri na kuwaheshimu, ila cha msingi aoe na ninamuombea kwa Mwenyezi Mungu apate mchumba wa kumuoa, awe mke mwema mwenye kupenda ndugu zake na inshaallah namuombea dua mwanangu aoe kabla sijafa,’’ alisema Mama Dangote.


 


TUJIKUMBUSHE


Mondi kwenye moja ya mikutano yake na waandishi wa habari kuwa miezi miwili iliyopita alikaririwa akisema kuwa, Oktoba 2, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa, lazima aoe, lakini mambo yamekuwa tofauti.


 


Miaka ya nyuma, Magazeti ya Pendwa ya Global Publishers yaliwahi kuchapisha habari mbalimbali zilizokuwa zikimhusisha Mondi na jamii hiyo ya siri ambapo nyingine zilikuwa na ushahidi wa picha za baadhi ya viongozi wa jamii hiyo. Mondi mwenyewe hakuwahi kukanusha wala kukubali kujihusisha na jamii hiyo huku baadhi ya mavazi yake anayopendelea kuyavaa yakiwa yanahusishwa na jamii hiyo.


 


WATOTO


Mondi ambaye ni baba wa watoto wanne aliozaa na wanawake tofauti, Zari, Hamisa na Tanasha, amekuwa akihusishwa kuwa na wachumba tofautitofauti ambao anatarajia kuwaoa akiwemo mrembo na ‘mwanasosholaiti’ kutokea nchini Rwanda, Mbabazi Shadia ‘Shaddy Boo’.