MTOTO mzuri kunako Bongo Fleva, Lulu Eugen ‘Amber Lulu’ amewapa za chembe baadhi ya wanaume wanaopendwa kulelewa almaarufu wanaume-marioo.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na Ngoma ya Kiboko ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, hatamani kutembea na mwanaume wa Kibongo kutokana na njaa walizonazo.
“Jamani mimi sitamani ku-date (kutoka kimapenzi) na mwanaume wa Kibongo kwa sababu wana njaa sana na wanapenda kulelewa. Unakuta mwanaume anaomba pesa mpaka mtu unajisikia kizunguzungu,” anasema Amber Lulu asiyeishiwa habari na vituko mjini ambaye ndoto yake kubwa ni kuzaa na staa wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.