Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya TUJUZANE

Android ===> GooglePlay


Mgombea Ubunge kupitia Chama cha ACT wazalendo Jimbo la Kigoma mjini Zitto Zuberi Kabwe amewahakikishia wananchi wa Jimbo hilo kuwajengea Soko kubwa Ili kuongeza uchumi Wa kibiashara jimboni Kigoma mini. 

Akizungumza na wananchi hao hii Leo Katika Kampeni za kumuombea kura Diwani Wa Kata Hiyo ndg Husein kalyango Zito amesema kuwa kumekuwa na changamoto kwa wafanya biashara  juu ya Biashara zao jimboni humo.

Aidha amesema kuwa Soko hilo La mkoa litajengwa Kata ya gungu kutokana na changamoto ya wenye maeneo mengine kudai fidia hivyo Hali iliyopelekea Soko hill kujengwa gungu.

Hata hivyo amesema tayari Bandari mbili zimeanza kujengwa ujiji na kibirizi  hivyo watu wakigoma na nchi jirani kunufaika na huduma Hiyo. 

Vilevile amewaomba wananchi kumchagua Diwani Wa Act Kata ya Kigoma mjini Husein Kalyango kwani amekuwa akifanya kazi ya Kusimamia miradi na ujenzi Wa miundo mbinu vizuri ikiwemo Barabara. 

Sanjari na hayo amewaomba wananchi kujitokeza kwa Wingi kupiga kura tarehe 28 oktoba mwaka huu na kuwasihi wananchi kuhakikisha karatasi ya kupiga kura ina muhuri Wa tume ya uchaguzi.