Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemsimamisha mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad   kutofanya mikutano ya kampeni za Urais kwa siku 5 baada ya kuonekana na kosa la uvunjifu wa maadili.

Akitangaza maamuzi ya Kamati ya maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar Katibu wa Kamati hiyo ya Maadili Khamis Issa Khamis amesema tume  ilipokea malalmiko kutoka kwa mgombea wa Urais wa chama cha Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir dhidi ya mgombea Maalim Seif ya kuhamasisha wananchama wake wakapige kura siku ya kura ya awali.

Katibu wa kamati amesema kamati ilisikiliza hoja zote na kuona kuwa mgombea Maalim Seif ametenda kosa hilo na kumpa adhabu kwa mujibu  wa sheria kifungu cha 23 D za kanuni za maadili.

Kamati hiyo ya maadili imetoa fursa kwa Maliam Seif kukata rufaa endapo haajridhika na mammzui hayo