KAMPUNI ya YARA Tanzania, inayotengeneza na kusambaza Mbolea nchini imezindua mbolea mpya inayojulikana kama MiCROP yenye lengo la kuwasaidia wakulima wadogo wa mahindi na mpunga kukuza mazao yao.

Mbolea hiyo mpya imezinduliwa Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wasambazaji wa bidhaa za YARA.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA Tanzania, Bw. Winston Odhiambo alisema MiCROP ni mbolea yenye mchanganyiko wa virutubisho vya zinc na Sulphur vinavyohitajika na mmea katika mfumo huo.

Alitoa wito kwa wakulima wachangamkie mbolea hii ya MiCROP kwa kilimo bora Zaidi na kuongeza kuwa mbolea hiyo itasambazwa nchi nzima.

Baadhi ya Wasambazaji na Mawakala wa Mbolea za YARA wameishuru kwa kuwa karibu na Wakulima na Wasambazaji, ili kukuza mazao kwa Wakulima na kuboresha maisha yao

Yara inazalisha mbolea zenye ubora zinazopatikana kila mahali na nyakati zote wakulima wa Afrika wanapozihitaji na inafanya kazi kwa ubia na taasisi za wakulima wenyeji,vikundi vya kijamii,na asasi zisizo za kiserikali kutoa elimu, majawabu ya lishe ya mimea na kuboresha maisha yao.

The post YARA yazindua mbolea ya MiCROP (+Video) appeared first on Bongo5.com.