Mwanamume wa Tunisia aliyewaua watu watatu katika ndanoi ya kanisa, Ufaransa aliwasili barani Ulaya hivi karibuni, maafisa wanasema.

Mshukiwa, 21, alikuwa na nyaraka za Shirika la Msalaba Mwekundu la Italia, alizopewa alipowasili nchini humo kupitia boti la wahamiaji kisiwani Lampedusa mwezi uliopita. Alipigwa risasi na polisi na kwasasa yuko katika hali mahututi.

Mmoja wa waathiriwa wa shambulio la kuchomwa kisi siku ya Alhamisi katika kanisa la Notre-Dame basilica mjini Nice karibu “akatwe kichwa”.

Rais Emmanuel Macron amesema lilikuwa “shambulizi la kigaidi”.

Bw. Macron amesema idadi ya polisi imeongezwa na wamepelekwa kutoa ulinzi katika maeneo ya umma- kama vile makanisa na shule – na idadi hiyo imeongezwa kutoka 3,000 hadi 7,000. Waendesha mashtaka wa kukabiliana na ugaidi wameanzisha uchunguzi huku Ufaransa ikiimarisha usalama wake wa kitaifa.

Shambulio la kisu la siku ya Alhamisi katika mji wa kusini mwa Ufaransa limezua hofu baada ya shambulio lingine kama hilo kutokea mapema mwezi huu karibu na shule kaskazini magharibi mwa mji wa Paris. Samuel Paty, mwalimu alikatwa kichwa siku kadhaa baada ya kuonesha vikaragosi vya utata kuhusu Mtume Muhammad kwa baadhi ya wanafunzi.

Mshukiwa alizuiliwa dakika chache baada ya shambulio la basilica
Mshukiwa alishikwa dakika chache baada ya shambulio la basilica

Mauaji hayo yamezua hali ya taharuki nchini Ufaransa. Bw. Macron ametetea uhuru wa kuchapishwa kwa katuni huku jaribio la serikali kukabiliana na visa vya waislamu wenye itikadi kali ikiighadhabisha Uturuki na nchi zilizo na idadi kubwa ya Waislamu.

Mshukiwa wa shambuli la Nice alisikika akisema kwa sauti maeneno “Allahu Akbar” (Mungu ni mkubwa) mara kadha kabala apigwe risasi na polisi.

Mshambuliaji huyo alipatikana na nakala ya Quran, simu mbili na kisu cha inchi 30, alisema mkuu wa waendesha mashtaka wanaokabiliana na ugaidi Ufaransa-Fran├žois Ricard.

“Pia tulipata begi lililoachwa na mshambuliaji huyo. Kanda na begi hilo kulikuwa na visu viwili ambavyo havikuwa vimetumiwa,” aliongeza.

Vyanzo vya polisi vimemtambulisha mshambuliaji huyo kama Brahim Aouissaoui.

Mshukiwa yuko katika hali mahututi, BW. Ricard alisema.

Akizungumza baada ya kuzuru eneo la tukio mjini Nice, Rais Macron alisema : “Ikiwa tunashambuliwa tena kutokana na maadili yetu: uhuru wa kujieleza na uwezo wa kuamini chochote kinawezekana katika ardhi yetu na kuamini kwa uhuru na kutokubali roho yoyote ya ugaidi

“Nasma kwa uwazi kwa mara nyingine tena: Hatutasalimu amri.”

Map showing the location of the attack in Nice

The post Yaelezwa aliyeshambulia kanisa nchini Ufaransa alitoka Tunisia appeared first on Bongo5.com.