Issa Mtuwa – Dodoma
Kampuni Sita zinazozalisha Saruji na Moja inayozalisha Mbolea yamekutana na kujadili na  Serikali kuhusu tozo mbalimbali za Usafirishaji (Clearance fee) na tozo za Ukaguzi (Inspection fee).

Lengo la kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, ni kujadili na kupitia (Review) tozo ya usafirishaji (Clearance fee) na tozo ya Ukaguzi (Inspection fee).   Wamesema tozo ya usafirishaji inatozwa na wizara mbalibali kama vile Madini, Kilimo na Viwanda na Biasha kiasi kwamba inakuwa kero na kuiomba Wizara ya Madini, tozo hiyo ielekezwe kwenye wizara moja, huku tozo la Ukaguzi ifutwe ama ipunguzwe.  

Mjadala huo umefanyika Octoba 7, 2020 Jiji Dodoma ukiwahusisha wataalam mbalimba akiwemo Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Makamishna Wasaidizi wa Madani, Maafisa mbalimbali wa Tume ya Madini na Maafisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Akizungumzia Prof. Msanjila  kuhusu malipo ya tozo kufutwa au kupunguza, alisema, Serikali haiwezi kuziondoa kwa sababu zimepangwa kwa mujibu wa sheria na zilijadiliwa kwa mapana na wadau mbalibali na kufiki maamuzi hayo.  Ameongeza kuwa mabadiliko haya yanahitaji mjadala mkubwa na wadau wengi.

Ameongeza kuwa, jambo la kujadili ni suala la kutotwa tozo ya aina moja kwa wizara kadhaa, alisema atalishugulikia na atakaa na Makatibu Wakuu wenzake wa wizara husika kuona namna ya kulitatua ili kuondoa kero hiyo. “Andikeni kwa maandishi mniletee muanishe hizo kero na mimi nitawaita Makatibu wenzangu tutakaa na kujadili,” alisema Prof.Msanjila. Serikali inahitaji Wawekezaji na Wawekezajizi waisaidie Serikali ili iweze kutoa huduma kwa Wananchi hivyo kulipa tozo ni muhimu sana.

Mmoja kutoka kwa Kampuni hizo, ambae ni Mwanasheria Mkuu wa Kampuni ya Mbeya Cement, Emmanuel Salla, alisema maombi yao yalilenga kujadili na kuptia (Review) tozo za usafirishaji na tozo ya ukaguzi ili wao waweze kupunguza bei ya bidhaa inayokwenda kwa wananchi.

Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement, Isaac Lupokela, alisema, “Tumekuwa na mkutano wenye tija ambao umefungua wigo mpana katika kuhakikisha maendeleo ya Viwanda na Serikali. Pongezi kwa Serikali kwa kuwa supportive sana. Ni mabadiliko makubwa katika taifa tumeyaona na tunapongeza,” alisema Lupokea.

Miongoni mwa Kampuni zinazozalisha Saruji na Mbolea ni; Dangote, Twiga Cement, Tanga Cement, Mbeya Cement, Lake Cement, Maweni Limstone, na Minjingu.