Msanii wa muziki Bongo, Whozu amesema kuwa mpenzi wake, Tunda kwa sasa ameamua kuachana kabisa na drama za kwenye mitandao ya kijamii.

Kauli ya Whozu inakuja mara baada ya hivi karibuni kuibuka stori kuwa Tunda karudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Young Dee kitu ambacho mrembo huyu pia alikikanusha vikali.


“Yeye mwenyewe amechoka, kwanini aendelee kuwepo kwenye mambo ambayo hayamjengii, yanambomoa kila siku. Vinamchafulia brand yake na ana vitu vingi vya kufanya, so kwanini aendelee na mambo hayo,” Whozu ameiambia Wasafi TV.


Kwa sasa Whozu anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Aaaah Wapi ambao ameshirikiana na Baddest 47