Shirika la kutetea haki la Amnesty International limesema karibu watu 50 wameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya kupinga serikali nchini Guinea mwaka jana.
Ripoti mpya ya shirika hilo limelaumu vikosi vya usalama kwa kutekeleza mauaji ya kiholela.
Baadhi ya waandamanaji walipigwa risasi wakiandamana dhidi ya hatua ya Rais Alpha Condé kutaka kusalia madarakani kwa muhula wa tatu.
Ripoti hiyo pia imeangazia jinsi watu 200 walivyojeruhiwa na wengine 70 kuzuiliwa kinyume cha sheria.
Uchaguzi wa urais utafanyika nchi humo baadaye mwezi Oktoba.
The post Watu 50 wameuawa kutokana na maandamano nchini Guinea (+Video) appeared first on Bongo5.com.