Matokeo ya urais yaliyotangazwa leo usiku Ijumaa Oktoba 30, 2020 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yanaonyesha kuwa Watanzania milioni 14.8 sawa na asilimia 49.8 hawakujitokeza kupiga kura.

Idadi hiyo ya watu milioni 14.8 ni kati ya Watanzania milioni 29.8 waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.

Uwiano huo wa watu ambao hawakujitokeza ni mkubwa ikilinganishwa na asilimia 33 ya ambao hawakujitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hata hivyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 waliojiandikisha kupiga kura walikuwa milioni 25.5.

Leo NEC imemtangaza mgombea wa CCM, John Magufuli

kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata kura 12,516,252 sawa na asilimia 84.4 kati ya kura halali 14,830,195.

Kwa mujibu wa matokeo hayo mgombea wa Chadema, Tundu Lissu amekuwa mshindi wa pili baada ya kupata kura 1,933,271 na kufuatiwa na mgombea kupitia ACT- Wazalendo, Bernard Membe aliyepata kura 81,129 na Leopord Mahona wa NRA kura 80,787.

The post Watanzania milioni 14.8 hawajapiga kura appeared first on Bongo5.com.