Mchakato wa kutangaza matokeo ya washindi wa uchaguzi nchini Tanzania yanaendelea kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini Tanzania.

Watanzania wameshuhudia anguko la wapinzani kwenye ngome zao mbalimbali zikinyakuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi za udiwani na ubunge.

Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema ambaye pia alikuwa mbunge wa Jimbo la Hai huko Moshi. Freeman Mbowe ameshindwa kutetea kiti chake, baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura na mgombea wa CCM, Saashisha Mafuwe.

Saasisha Mafuwe CCM ameongoza kwa kura 89,786 dhidi ya kura 27,684 za Freeman Mbowe.

Freeman Mbowe amekuwa mbunge wa Chadema kwa miaka 10

Zitto Kabwe:

Alikuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo. Zitto amekuwa mbunge kwa miaka 15, miaka 10 jimbo la Kigoma Kaskazini, na miaka mitano jimbo la Kigoma mjini ambalo alikuwa akitetea kiti chake.

Zitto Kabwe

Zitto amebwagwa na mgombea wa CCM Kilumbe Ng’enda. Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Ng’enda amepata kura 27,688 huku Zitto akipata kura 20,600.

Joseph Mbilinyi

Sugu

Joseph Mbilinyi maarufu Mr.Two au Sugu amekuwa mbunge wa Mbeya mjini kupitia chama cha upinzani cha chadema nchini humo tangu mwaka 2010 mpaka 2020.

Mgombea wa Chama cha mapinduzi katika jimbo la Mbeya mjini Dkt. Tulia Akson ameibuka mshindi katika uchaguzi wa eneo hilo.

Dkt Tulia Akson alimshinda Sugu kwa kura 75,225 dhidi ya kura 37,591 za Joseph Mbilinyi.

Joseph Haule:

jay

Msanii wa Bongo Fleva Joseph Haule maarufu Profesa Jay wa chama cha CHADEMA ameshindwa kutetea jimbo la Mikumi, ambalo alikuwa mbunge kwa kipindi cha miaka mitano.

Profesa Jay amepata kura 17,375 huku mpinzani wake Denis Lazaro wa chama cha CCM akiibuka mshindi kwa kupata kura 31,411.

Profesa Jay alipata umaarufu mkubwa kwa kibao chake cha ‘ndio mzee’.

Godbless Lema

Godbless Lema wa Chadema ameshindwa kutetea jimbo lake la Arusha mjini baada ya kushindwa na mgombea wa CCM, Mrisho Gamba aliyepata kura 82,480 na huku Lema akiwa na kura 46,489.

Lema amekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka 10.

HALIMA MDEE

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kawe amemtangaza Askofu Josephat Gwajima wa CCM kuwa ndiye mshindi wa jimbo hilo kwa kupata kura 194,833 na kumshinda Halima Mdee wa CHADEMA aliyepata kura 32,524.

PETER MSIGWA

MSIGWA APIGWA CHINI MSAMBATAVANGU ASHINDA IRINGA MJINI: Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Iringa Mjini amemtangaza Jesca Msambatavangu wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 36,034 akifuatiwa na Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema aliyepata kura 19,331.

 

LAZARO NYALANDU

Mgombea ubunge kupitia Chadema Lazaro Nyarandu ameshindwa ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini baada ya kushindwa na mgombea wa CCM, Rashid Mandoa aliyepata kura 43,847.

ESTER MATIKO

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tarime Mjini, Ester Matiko ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kushindwa na mshindani wake, Michael Kembaki wa Chama cha Mapinduzi .

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Elias Ntiruhungwa amesema kuwa Kembaki ameshinda kwa kupata kura 18,235 huku Matiko akipata kura 10,873 na mgombea wa NCCR Mageuzi, Ester Nyagabona akipata kura 143.

ESTER BULAYA

Robert Maboto wa CCM ameshinda kiti cha ubunge Jimbo la Bunda Mjini akipata kura 31,129 dhidi ya Ester Bulaya wa CHADEMA aliyepata kura 13,258.

 

Mbali na hilo Chama Tawala mpaka sasa hivi kimepata viti vya Ubunge kwa vyama vya siasa hadi sasa kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Chama Cha Mapinduzi (CCM): Viti 188 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA): Viti 1 Civic United Front (CUF: Viti 1

The post Wanasiasa maarufu waliopoteza majimbo yao Tanzania, matokeo ya mwanzo CCM yashinda majimbo 188 upinzania 2 appeared first on Bongo5.com.