Samirah Yusuph
Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa ardhini LATRA  imesema kuna haja ya wawekezaji kuwekeza katika sekta ya usafirishaji mkoani Simiyu ili kuondoa adha ya kukosekana kwa huduma za usafiri ndani ya mji pamoja na gharama kubwa za usafiri kwa mtu mmoja mmoja ambazo kwa sasa zipo juu.

LATRA ilitoa pendekezo hilo ilipokutana na wadau wa usafirishaji ardhini  mkoani humo na kujadili changamoto za usafirishaji ikiwemo kutokuwepo kwa maegesho ya magari kwa ajili kubeba na kushusha abiria pamoja na watumiaji wa vyombo vya usafiri kukosa elimu ya usalama Barabarani  

Akibainisha changamoto alizoziona katika mkao huo Meneja wa udhibiti usafiri wa barabara Leo Ngowi alisema kuwa  hakuna usafiri katikati ya mji huo.

Alisema Hakuna  usafiri kabisa katikati ya mji na hakuna maeneo ya maegesho hali inayopelekea nauli kuwa kubwa kutokana na wasafirishaji kukosa muongozo wa malipo kwa kituo kwa kituo.

Upungufu wa vyombo vya usafirishaji katika maeneo mengi ya mkoa ni moja kati ya mambo yaliyotajwa kama adha kwa wananchi

wadau wa usafirishaji ardhini wametoa ushauri kwa mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini LATRA kusajiri vyombo vingi na kuvipangia safari katika maeneo yenye uhaba wa vyombo vya usafiri kama alivyoeleza Peter Majira mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Simiyu.

Majira alisema kuwa wanajua kuna magari ambayo ni mabovu lakini wakiyaondoa yote barabarani wananchi watatumia usafiri gani, hivyo ni mhimu kwa wadau usafiri kuweza kuwekeza zaidi ili kuweza kumaliza kero adha hii,

Wakala wa barabara za vijijini na mjini TARURA ni moja ya wadau walioshiriki kikao hicho cha kujadili changamoto hizo hivyo muwakilishi wa mratibu wa wakala huyo Roda Ngungi alisema kuwa kuongeza mtandao wa barabara ni njia pekee zinazoweza kuishinda changamoto hiyo.