Rihanna, Kanye West na Nicki Minaj ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamejitokeza uunha mkono maandamano dhidi ya ukatili wa polisi nchini Nigeria. Lakini waandamanaji walimkaripia Beyoncé alipozungumzia suala hilo. Kwanini?

Wasanii kadhaa wa kimataifa wamejitokeza kuunga mkono maandamano hayo

Rihanna aliweka kwenye mtandao wake wa Twitter picha ya bendera ya Nigeria iliyokuwa na damu na kuambatanisha maneno: “Moyo wangu umevunjika kutokana na matukio yanayoendelea Nigeria.

Nikki Minaj alizungumza na waandamanaji moja kwa moja katika Twitter yake, akisema: “Sauti yenu inasikika”.

Halafu ikafuata kauli ya Beyoncé

Kupitia shirika lake la misaada la, BeyGood, alisema: “Nimevunjika moyo kuona unyama usiokuwa na maana unafanyika nchini Nigeria … tunashirikiana na miungano kutoa huduma za dharura za afya, chakula na malazi. “

Ruka Twitter ujumbe, 4

Mwisho wa Twitter ujumbe, 4

Kauli hiyo haikupokelewa vyema na waandamanaji.

“Nani alimwambia Beyoncé tuna njaa?” alitoa maoni mjasiriamali wa kidijitali Papi Jay.

Ruka Twitter ujumbe, 5

Mwisho wa Twitter ujumbe, 5

Maoni yake yaliungwa mkono na muuzaji wa vipodozi Mercy Ehimare. “kuna mtu anaweza kumwambia mwanamke huyu hatuna njaa??????? Tunahitaji msaada kupigania haki yetu, “alijibu.

Ruka Twitter ujumbe, 6

Mwisho wa Twitter ujumbe, 6

Wafuatiliaji wa mtandao wa Twitter walighadhabishwa na kauli ya Beyoncé iliyoashiria wao ni maskini.

Hiyo sio jinsi waandishi wa habari wa Nigeria walivyowaelezea watu ambao walianzisha maandamano hayo mtandaoni.

Badala yake waliamua kuwaita watu wenye “ushawishi katika mtandao ya kijamii”.

Siku za mwanzo wa maaandamano hayo, mwandishi wa BBC Nduka Orjinmo aliwataja watu waliokuwa wakiandamana kama ”kama vijana ambao baadhi yao wameweka rangi nywele zao, wengine wakiwa wametoboa pua na kutchora tattoo kwenye miili yao”.

Pia kulikuwa na watu kama mwanaharakati Rinu Oduala, ambaye alikuwa amewashawishi waandamanaji wengine kukesha nje ya majengo ya serikali mjini Lagos mwezi Oktoba tarehe 7.

Kwa hivyo wakati huu, waandamanaji walitaka tu kupaziwa sauti ujumbe wao kuhusu ukatili dhidi ya polisi

Beyonc̩ ana wafuatiliwa na zaidi ya watu milioni 15 katika akaunti yake binafsi ya Twittter РHii inamaanisha ujumbe atakaotuma utawafafikia watu wengi.

Lakini walighadhabishwa na ujumbe wa Beyoncé anasema dor_gd, ambaye alisema aliuamua kuwaunga mkono maandamano hayo kupitia akaunti ya shirika lake la misaada.

Ruka Twitter ujumbe, 7

Mwisho wa Twitter ujumbe, 7

Wakosoaji pia walisema Beyoncé alichelewa kujiunga na maandamano hayo

Ruka Twitter ujumbe, 8

Mwisho wa Twitter ujumbe, 8

Maandamano yalianza wiki kadhaa kabla aamue kujiunga na wimbi la pili la watu maarufu kuonnyesha uungaji mkono wake.

Watu kama muigizaji wa Star Wars, John Boyega, Mchezaji wa Arsenal Mesut Özilna rappa Kanye West tayari walikuwa wametangazakuunga mkono maandamano hayo kwenye Twitter wiki moja kabla yake..

Ruka Twitter ujumbe, 9

Mwisho wa Twitter ujumbe, 9

Ruka Twitter ujumbe, 10

Mwisho wa Twitter ujumbe, 10

Ruka Twitter ujumbe, 11

Mwisho wa Twitter ujumbe, 11

Wakati alipotweet, maandamano ya amani yalikuwa tayari yamegeuka kuw aya umwagikaji damu.

Kwa nini watu wanaandamana?

Maandamano yalianza karibu wiki mbili zilizopita kushinikza kuvunjiliwa mbali kwa kitengo maalum cha polisi cha kukabiliana na wizi wa mabavu (Sars).

Kitengo hicho kimetuhumiwa kuwazuilia watu kinyume cha sheria, kuwanyanyasa na kuwa kuwapiga risasi na kilivunjwa na Rais Muhammadu Buhari Oktoba tarehe 11.

Lakini maandamano yameendelea kushuhudiwa katika maeneo kote nchini, miito ya kutaka huduma za usalama kufanyiwa mageuzi pamoja na serikali kwa ujumla.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, kumeshuhudiwa ongezeko la watu wanaounga mkono maandamano ya Nigeria kupitia mtandao wa Twitter, kupitia hashtag tofauti, lakini ile iliyopata umaarufu ni ya #EndSARS.

Maandamano hayo wakati mwingine yamekubwa na vurugu. Siku ya Jumanne shirika la kutetea haki la Amnesty International lilisema makundi ya watu waliojihami yalishambulia watu katika mji mkuu, Abuja.

Waandamanaji wakiinua mabango
Maelezo ya picha,Kampeni ya #EndSARS imepata umaarufu kwenye mitandao kote ulimwenguni

Kwa upande wao pilisi wamewalaumu watu kwa “kujifanya” waandamanaji na kuiba silaha na kuchoma moto ofisi za polisi katika jimbo la kusini la Edo.

Katika hotuba ya video siku ya Jumatatu, Rais Buhari alisema maafisa wa polisi waliojihusisha na visa vya uvunjifu wa sheria watachukuliwa hatua za kisheria na kuongeza kwamba kuvunjwa kwa kitengo cha Sars ni “hatua ya kwanza katika jitahada za serikali za kufanya mageuzi katika idara ya polisi”.

The post Waandamanaji Nigeria wamvaa Beyonce baada ya kusema wasaidiwe chakula, aliyemwambia tuna njaa ni nani appeared first on Bongo5.com.