Wanachama wanne Wa Chama cha ACT Wazalendo wamekabidhi kadi  zao jana katika mkutano Wa CCM kata ya Uvinza Mkoani Kigoma.


Wamekabidhi kadi hizo mbele ya mgombea ubunge  Jimbo la Kigoma Kusini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Nashon Bidyanguze na kuahidi kukitumikia Chama cha Mapinduzi kwa uadilifu


Kwa upande wake Mwenyekiti Wa siasa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Emanuel Karayenga ameasema kuwa Chama cha Mapinduzi hakina ubabaishaji kinafanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.


" Ukiona mtu anahamia CCM usifikirie kafuata  rangi ya kijani  sisi tunafuata ilani ya Chama chetu ndugu zangu msijalibu kuonja sumu"


Ashura Shaban na Moshi Magongo  ni miongo mwa wananchi waliohudhulia mkutano huo na kuahidi watahakikisha wanachagua kiongozi aliyebora kwa maslahi ya nchi kwani Sera ya Chama cha Mapinduzi ni Sera zenye maslahi kwa jamii.


Hata hivyo Mgombea Ubunge  Jimbo la Kigoma Kusini Nashon Bidyanguze amewaahidi kuwa endapo watampa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha anashirikiana nao kujenga barabara ,solo la Wilaya, Stendi na kuhakikisha miundombinu shuleni inaimarika.