Kundi la muziki nchini Kenya Sauti Sol linatajwa kuwa na nyimbo 300 ambazo wameshirikiana na mkali toka Nigeria, Wizkid.


Taarifa hiyo imetufikia kupitia Sandra Bartonjo ambaye ni muandaaji wa matamasha na mdau mkubwa wa muziki nchini Kenya. Kwenye podcast yake alisema Sauti Sol na Wizkid wana nyimbo 300 ambazo hazijatoka na nyingi walizirekodi kipindi Wizkid amekuja Kenya kwa ajili ya onesho lake.


"Wizkid anafikiria tofauti sana na wenzake. Nilipata nafasi ya kutumia muda wangu na yeye, namna alivyojipanga na namna akili yake inafanya kazi ni kitu cha kipekee sana. Hawezi kufanya kazi na wewe. Ni lazima uendane na uchizi wake, hivyo mpaka sasa Sauti Sol wana nyimbo 300 ambazo hazijatoka wakiwa na Wizkid." alisema Sandra Bartonjo.