Baada ya Alikiba kutoa wimbo wa Vijembe kwa Diamond wengi waliupokea vibaya ikiwemo Mashabiki zake ambao hawajamzoea Alikiba wa aina hiyo mpaka sasa wimbo huo umepotea na hausikiki popote nchini.


Wimbo huo umepotea kwa sababu mbalimbali sababu kubwa ni Diamond kutokujibu vijembe hivyo, Endapo angejibu basi ingekuwa ni Promo tosha ya wimbo huo na wangezua Mjadala Mitandaoni na mitaani.


Yawezekana lengo la Alikiba kutoa wimbo wa Diss ilikuwa ajibiwe na Diamond ili iwe kiki kwake lkn Diamond kashtukia mchezo kakaa kimya kama haujausikia huo wimbo yaani kaupuuza kaamua kutokuupa kiki.


Kuna kipindi Diamond alikuwa anamdiss sana Kiba na Alikiba alikuwa hana muda wa kujibu, sasa amemiss diss ili zimpush kisanaa lkn amechelewa maana Diamond kashagundua kuwa kumdiss Alikiba ni kumpa kiki zaidi.


Kiba akae Chini atulize kichwa asifanye muziki kwa Hasira lazima akubali kuwa kwa sasa kwenye soko la Ushindani ni Diamond na Harmonize.