Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kukomeshwa kile alichokiita “ukatili” wa polisi nchini Nigeria, ambayo imekumbwa na maandamano kwa wiki mbili sasa.

Nigeria: UN slams ′brutality′ against #EndSARS protesters | News | DW | 21.10.2020

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema katika taarifa kuwa Guterres amevihimiza vikosi vya usalama kujizuia kwa wakati wote wakati akitoa wito kwa waandamanaji kuandamana kwa amani na kujiepusha na machafuko.

Guterres amesema watu waliokuwa na silaha ambao waliwafyatulia risasi za moto waandamamanaji wa amani jana usiku mjini Lagos walisababisha vifo kadhaa na majeruhi wengi.

Wakati huo huo, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel amelaani mauaji ya waandamanaji akitoa wito wa kupatikana haki. Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimeitaka mamlaka nchini Nigeria kuchunguza na kuwawajibisha waliohusika na matukio hayo.

 

The post Ukatili wa polisi ukomeshwe Nigeria – Umoja wa Mataifa appeared first on Bongo5.com.