Wapiga kura wana hadi mwendo wa saa kumi jioni kupiga kura. Matokeo yanatarajiwa kutangazwa ndani ya juma moja .nRais John Pombe magufuli ambaye chama chake cha mapinduzi CCM kimetawala Tanzania tangu uhuru 1961, anawania kwa muhula wa pili.

Mpinzani wake mkuu ni Tundu Lissu wa chama kikubwa cha upinzania Chadema , ambaye alinusurika mauaji miaka mitatu iliopita .

Alirudi kutoka Ubelgiji mwezi Julai ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu ya majeraha ya risasi.

Takriban wagombea 15 wanawania urais akiwemo aliyekuwa waziri wa masuala ya kigeni Bernard Membe.

The post Uchaguzi Tanzania 2020: Watanzania waanza kushiriki katika zoezi la kupiga kura appeared first on Bongo5.com.