Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amesema jaribio lolote lenye nia ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 na kutumia mabavu litapelekea watu kufikishwa Mahakama ya Kimataifa 'The Hague'
Amesema, "Kuna uchunguzi unaendelea, wa matukio yote ambayo yanafanyika na yameshafanyika. Kuna list (orodha) ya watu wanaoangaliwa"
Ameongeza kuwa, yeyote atakayetumia mbinu za kiharamia kuvuruga Uchaguzi na kusababisha maafa kwa Watanzania anajiingiza mwenyewe katika orodha hiyo