Rais Donald Trump na mshindani wake Joe Biden wamepambana katika mdahalo wa pili na wa mwisho wa kampeni za kugombea urais uliofanyika kwenye mji wa Nashville katika jimbo la kusini la Tennessse.

Biden aliyekuwa makamu wa rais wa Marekani hapo awali, amesema Trump hafai tena kuwa rais wa nchi hiyo kutokana na vifo vya wamarekani zaidi ya laki mbili viliyvosabaishwa na maambukizi ya virusi vya corona. Amesema rais Trump hana mkakati wowote juu ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo. Trump alijibu kwa kusema kwamba wamarekani wanapaswa kutoka nje na kufanya kazi.

Katika mdahalo wa leo uliofanyika kwa staha, tofauti na ule wa kwanza, rais Trump amedai kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona inakaribia kupatikana nchini Marekani. Kwenye mdahalo huo rais Trump pia alimshutumu Biden kutokana na mahusiano ya mtoto wake nchini Ukraine. Trump amedai kwamba akina Biden wamejipatia mamilioni kutoka Ukraine. Trump alirudia tena kumtuhumu Biden na mtoto wake Hunter kwamba walifanya vitendo visivyo vya maadili nchini China na Ukraine ingawa hakuna ushahidi uliothibitishwa kuhusiana na madai hayo. Vile vileTrumpalimtuhumu Biden kwamba amepokea fedha kutoka Urusi.

Kushoto: rais wa Marekani Donald Trump.Kulia mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden (Morry Gash/Reuters)Kushoto: rais wa Marekani Donald Trump.Kulia mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden

Joe Biden amekanusha madai hayo na alii tetea familia yake. Amesisitiza kwamba hakuwahi kupokea hata senti moja kutoka nchi ya kigeni, amesema Trump anajaribu kuwavuruga Wamarekani. Biden alibaini kuwa ameweka wazi mrejesho wa ushuru aliolipa kwa kipindi cha miaka 22, ambapo hakuna ushahidi iwapo amewahi kupokea pesa kutoka kwa chanzo chochote cha kigeni katika maisha yake.

Biden alimtaka Trump aonyeshe marejesho yake ya kodi badala ya kuwapakazia wenzake maneno yasiyo na ushahidi Trump akajibu kuwa ataweka bayana haraka iwezekanavyo. na kwamba alilipa kodi mapema kabla ya wakati katika miaka kadhaa iliyopita, amesema alilipa mamilioni ya dola.

Wakati zimebakia siku11 kabla ya uchaguzi, rais Trump anayewania muhula wa pili amejitetea juu ya madai ya kuwa na akiba ya benki nchini China.Trump amesema akiba hiyo ya benki ni ya toka mwaka 2010 wakati alipokuwa mfanyabiashara.

Katika siku za hivi karibuni, maafisa wa Marekani waliripoti kuwa wadukuzi wa Urusi wamelenga mitandao ya serikali za majimbo kadhaa na ile ya serikali za mitaa nchini Marekani na kuiba data kutoka kwenye seva mbili. Maafisa hao pia wameituhumu Iran kwa kuhusika na kutumiwa barua pepe wapiga kura wengi wa chama cha Democratic katika majimbo kadhaa barua pepe zilizowashinikiza au kuwatisha wampigie kura rais Donald Trump.

Juu ya madai ya kuingiliwa kati uchaguzi wa Marekani makamu wa rais wa zamani Joe Biden amesema ameweka wazi kuwa nchi yoyote, bila kujali ni ya nani, itakapobainika kuingilia kati uchaguzi wa Marekani, basi, italipa gharama kubwa.

Mdahalo huo ulioonekana moja kwa moja kwenye televisheni kutoka Nashville, Tennessee, ulikuwa ni fursa ya mwisho kwa Trump wa chama cha Republican kuwasihi wapuga kura na kuweka mkazo kwenye kampeni iliyotawaliwa na janga la COVID -19 ambalo limesababisha vifo vya zaidi ya watu laki mbili na elfu ishirni nchini Marekani.

Kura za maoni zinaonyesha Trump yuko nyuma ya Biden, ingawa mashindano ni makali katika baadhi ya majimbo yanayogombewa ambayo yana nafasi kubwa ya kubadili mambo kwenye kinyang’anyiro hicho cha urais nchini Marekani.

The post Trump, Biden uso kwa uso, walumbana kuhusu Corona appeared first on Bongo5.com.