Rais wa Marekani Donald Trump amerejea kwa kishindo katika Ikulu ya White House kuendelea na tiba ya virusi vya corona baada ya kulazwa hospitali kwa siku tatu.

Rais alitoa barakoa yake katoka roshani ya White House, ambako wafanyakazi kadhaa na washauri wake walipatikana na virusi hivi karibuni.

“Najihisi vyema sana!” Bw. Trump awali aliandika katika Twitter yake.”Usiogope Covid. Usiache itawale maisha yako.”

Zaidi ya watu milioni 7.4 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani. Virusi vya ugonjwa huo vimewaua takriban Wamarekani 210,000.

Maswali bado yanaibuliwa kuhusu ugonjwa wa Bw. Trump baada taarifa kinzani kutolewa wikendi iliyopoti kuhusu hali yake. Ukubwa wa mlipuko wa virusi katika Ikulu ya White House bado unaendelea kuwa kitendawili.

Nini kilifanyika Trump alipotoka hospitali?

Akiwa amevalia suti , tai na barakoa, Bw.Trump alitoka nje ya Hospitali ya kitaifa ya kijeshi ya Walter Reed mjini Washington DC Jumatatu usiku akikunja ngumi na kuinua mkono juu.

Asanteni sana,” alisema, akipuuza maswali kutoka kwa wanahabari, akiwemo mmoja aliyemuuliza: “Una uhakika hutasambaza virusi bila kujua bwana Rais?”

Baada ya safari fupi ya helikopta, Bw.Trump alipigwa picha akiwa peke yake kwenye roshani ya Truman katika Ikulu ya White House. Alivua barakoa, kisha akainua juu kidole gumba na baadae kupiga saluti ya mtindo wa kijeshi.

Saa chache baadae, aliweka ujumbe kwenye Twitter kama ishara kwamba anajiandaa kurejea kwenye msururu wa kampeni.

Muda mfupi kabla ya kuondoka hospitali, aliandika ujumbe kwenye Twitter yake na kusema: “Nitarudi kwe kampeni hivi karibuni!!! Taarifa feki zinaonesha kura feki za maoni.”

Bw.Trump anagombea muhula wa pili madarakani na atakabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden chini ya mwezi mmoja katika uchaguzi mkuu wa urais.

Akiwahusia Wamarekani wasiogope ugonjwa wa corona katika ujumbe wake wa awali kwenye Twitter siku ya Jumatatu, Bw. Trump aliongezea kusema: “Utawala wa Trump, umetengeza dawa na kujifunza mengi. Najihisi vyema zaidi kuliko miaka 20 iliyopita!!”

Madaktari wa Trump walisemaje?

Dakari wa White House Navy Cdr Sean Conley, siku ya Jumatatu alisema Bw. Trump “huenda hajapona kabisa”.

Lakini alisema madaktari wake wamekubaliana kuwa rais anaendelea kupata nafuu na “tunaunga mkono kurejea kwake salama nyumbani, ambako atapewa uangalizi wa hali ya juu wa kimatibabu wakati wote”.

Dkt Conley alikataa kujibu maswali kuhusu ni lini Bw. Trump alipokea matokeo ya kuonesha hana virusi au alifanyiwa tiba maalum. Alisema hatatoa maelezo zaidi kuhusu uchunguzi wa matibabu ya rais akitumia sheria ya faragha ya mgonjwa.

Daktari wa White House alithibitisha kuwa Bw. Trump anatumia tiba ya dexamethasone na kwamba anapewa dozi tatu ya dawa ya remdesivir. Alikuwa apewe dozi nyingine kabla ya kuondoka hospitali kurejea White House.

Alipoulizwa ikiwa ni salama kwa Bw. Trump kusafiri kwenda kwa shughuli za kampeni, Dk Conley alisema: “Tutaona.”

Pia alieleze hofu yake binafsi kwamba huenda aliambukizwa virusi alipokuwa ndani ya ndege ya Air Force One.

Lakini kundi la madaktari wa Bw. Trump limesisitiza mara kwa mara jinsi hali ya afya ya rais inavyoendelea kuimarika, katika mazungumzo na wanahabari siku ya Jumatatu.

“Tuna matumaini makubwa,” Dk Conley alisema, akiongeza kuwa Bw. Trump alipata tuba mapema.

“Ikiwa tutafanikiwa kuendelea kuwa naye hivi hadi Jumatatu [wiki ijayo] siku chache zilizosalia ni kuhakikisha tu yuoko sawa kabla ya kukamilisha tiba yake nasi tuvute pumzi.”

Hali ikoje baada ya mlipuko wa virusi White House?

Kutolewa kwa rais hospitali kunakuja wakati ambapo visa zaidi vya maambukizi vimeripotiwa miongoni mwa wafanyakazi wa White House.

Waziri wa Habari Kayleigh McEnany ni afisa wa ngazi ya juu wa karibu na rais kupatikana na virus via corona siku ya Jumatatu.

Vyombo vya Habari nchini Marekani vimeripoti kuwa wasaidizi wengine wawili wa waziri wa habari.

Bi McEnany alionekana akizungumza na wanahabari akiwa hajavalia barakoa siku ya Jumapili lakini amesema wanahapari hao wameorodheshwa na kitengo cha afya cha White House kama watu waliotangamana naye.

Washauri wakuu wa mke wa rais, Melania Trump, na Maseneta watatu wa Republican pia wamethibitishwa kuwaitiani na virus via corona.

Mke wa Trump, mwenye na umri wa miaka 50, amewekwa karantini White House, aliandika katika twitter yake: najihidi vyema [na] nitaendelea kupumzika nyumbani.

Karibu maafisa 12 wa ngazi ya juu waliotangamana na rais Trump wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona, wakiwamo pia maafisa wa ngazi ya chini.

Baadhi ya watu waliopatikana na virusi ni wale waliotangamana kwa karibu na Bw.

Trump walipohudhuria mkutano ndani ya White House mwezi Septemba tarehe 26. Mkutano huo unasadikiwa kuwa chimbuko la “mlipuko wa virusi” .

Ikulu ya White House haijatoa oradea kamili inayoonesha ni wafanyakai wangapi wamepatikana na virusi tangu Bw. Trump alipothibitishwa kuwa na corona.

Mtu wa hivi katibuni kupatikana na virusi alikuwa amehudhuria mkutano huo ambao rais alitumia kumtangaza mteuzi wake katika Mahakama ya juu zaidi nchini Marekani ni kiongozi mmoja wa kidini.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo wa White House, Mchungaji Greg Laurie piaalikuwa na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence katika matembezi ya maombi katika eneo la Washington DC.

View this post on Instagram

——————————————————————————-Rais wa Marekani Donald Trump amerejea kwa kishindo katika Ikulu ya White House kuendelea na tiba ya virusi vya corona baada ya kulazwa hospitali kwa siku tatu. Rais alitoa barakoa yake katoka roshani ya White House, ambako wafanyakazi kadhaa na washauri wake walipatikana na virusi hivi karibuni. "Najihisi vyema sana!" Bw. Trump awali aliandika katika Twitter yake."Usiogope Covid. Usiache itawale maisha yako." Zaidi ya watu milioni 7.4 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani. Virusi vya ugonjwa huo vimewaua takriban Wamarekani 210,000. Maswali bado yanaibuliwa kuhusu ugonjwa wa Bw. Trump baada taarifa kinzani kutolewa wikendi iliyopoti kuhusu hali yake. Ukubwa wa mlipuko wa virusi katika Ikulu ya White House bado unaendelea kuwa kitendawili. Nini kilifanyika Trump alipotoka hospitali? Akiwa amevalia suti , tai na barakoa, Bw.Trump alitoka nje ya Hospitali ya kitaifa ya kijeshi ya Walter Reed mjini Washington DC Jumatatu usiku akikunja ngumi na kuinua mkono juu. Asanteni sana," alisema, akipuuza maswali kutoka kwa wanahabari, akiwemo mmoja aliyemuuliza: "Una uhakika hutasambaza virusi bila kujua bwana Rais?" Baada ya safari fupi ya helikopta, Bw.Trump alipigwa picha akiwa peke yake kwenye roshani ya Truman katika Ikulu ya White House. Alivua barakoa, kisha akainua juu kidole gumba na baadae kupiga saluti ya mtindo wa kijeshi. Saa chache baadae, aliweka ujumbe kwenye Twitter kama ishara kwamba anajiandaa kurejea kwenye msururu wa kampeni. Muda mfupi kabla ya kuondoka hospitali, aliandika ujumbe kwenye Twitter yake na kusema: "Nitarudi kwe kampeni hivi karibuni!!! Taarifa feki zinaonesha kura feki za maoni." Bw.Trump anagombea muhula wa pili madarakani na atakabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden chini ya mwezi mmoja katika uchaguzi mkuu wa urais. Akiwahusia Wamarekani wasiogope ugonjwa wa corona katika ujumbe wake wa awali kwenye Twitter siku ya Jumatatu, Bw. Trump aliongezea kusema: "Utawala wa Trump, umetengeza dawa na kujifunza mengi. Najihisi vyema zaidi kuliko miaka 20 iliyopita!!" ( Via Trump on Twitter ) Written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Trump apuuzia mbali corona baada ya kutoka hospitali, Usiiogope pia usiiache ikutawale maisha yako (+Video) appeared first on Bongo5.com.