TAFUTENI pesa siyo majungu! Ndivyo unavyoweza kusema unapomzungumzia mtoto wa staa mkubwa wa muziki Bongo na bosi wa lebo ya muziki ya Wasafi Classic baby (Wcb), nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’.

Maisha anayoishi Princess Tiffah au Tiffah Dangote, mwenye umri wa miaka mitano, anawafunika mastaa kibao wa kike Bongo wanaopenda kujipaisha, ilhali wana hali mbaya kimaisha

Tiffah ni mtoto wa kwanza wa Mondi, ambaye amezaa na mwanamama mjasiriamali, raia wa nchini Uganda, mwenye maskani yake pale Durban, Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Tiffah ni miongoni mwa watoto maarufu zaidi Afrika Mashariki wanaoishi maisha ya kifahari, umaarufu wake aliupata tangu siku ya kwanza alipoliona jua.UbaLozi KaMa WoteTiffah anaongoza kuwa balozi wa makampuni mbalimbali, ikiwemo maduka ya nguo Bongo, kampuni ya huduma ya simu za mikononi, benki na mengineyo.

BATA ZA KISTAA

Tiffah ndiye rafiki kipenzi kwa mama yake (Zari) na amekuwa akipewa starehe au bata la kistaa.Kumekuwa na picha ambazo zinazomuonesha Tiffah akiwa katika hoteli kubwa akila bata na vyakula vya bei mbaya, kiasi kwamba kuna mastaa wa kike Bongo hawafikii levo hizo

Maisha ya Tiffah yamekuwa yakiwatoa wengi udenda na kuishia kumsifia kuwa nyota yake ni ya kistaa.“Kwenye orodha ya watoto wanaoishi kistaa, Tiffah hawezi kukosekana, maana anakula bata balaa,’’ aliandika mmoja wa wafuasi wa Tiffah kwenye ukurasa wake.

WAFUASI MTANDAONI

Tiffah ni mtoto ambaye anafuatiliwa zaidi mitandaoni, kwani ana wafuasi zaidi ya milioni 2.5 kwenye ukurasa wake wa Instagram.Ukurasa wake huo wa Instagram, umekuwa ukimuingizia mkwanja mrefu, hasa kutokana na matangazo yanayowekwa.

KUFURU YA BETHIDEI

Miezi miwili iliyopita, Tiffah alisherehekea sherehe yake ya kuzaliwa (birthday) ya kutimiza umri wa miaka mitano huko Durban nchini Afrika ya Kusini anakoishi na mama yake.Sherehe hiyo ilikuwa ni kufuru zaidi ya harusi, kwani ilitumia mamilioni ya pesa.

CHUMBA CHAKE USIPIME

Katika ukurasa wake wa Instagram, Tiffah ameposti picha zikionesha chumba chake cha kulala, ambacho kufuru yake usipime.Chumba hicho ni cha kifahari na hata kitanda anacholalia ni cha kistaa, jambo linalowafanya baadhi ya watu kumuonea gere.

MITUPIO YAKE

Mtoto huyo amekuwa akionekana kutupia pamba za ukweli, viatu na hata mikoba ya bei mbaya, ambayo ni ya kifahari zaidi kutoka kampuni kubwa za fasheni duniani.

NYOTA YA KUPENDWA

Mondi ana watoto wanne; Tiffah, Nillan, Dyllan na Naseeb Junior, lakini Tiffah anaonesha kupendwa zaidi na watu wa karibu kama baba, mama, bibi, ndugu zake na hata watu wa karibu wa Mondi.

Mama mzazi wa Mondi, Sanura Kassim ‘Sandra’, amekuwa akimposti Tiffah kwenye ukurasa wake wa Instagram na kummwagia sifa kedekede.

KIPAJI

Tiffah ni mtoto ambaye amejaaliwa kuwa na vipaji kadhaa kama vile uanamitindo, upishi, kuimba na kudansi.Mara nyingi amekuwa akiposti vipande vya video kwenye ukurasa wake wa Instagram, vikimuonesha manjonjo ya vipaji vyake kiasi cha kuzungumzwa mitandaoni kuwa, mtoto wa nyoka naye ni nyoka.