Samirah Yusuph
Simiyu. Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC kimenuia kumaliza changamoto kwa wawekezaji nchini kwa kuongeza ufanisi wa kiutendaji ikiwamo utoaji wa vibali mbalimbali, leseni na usajili wa miradi kwa haraka zaidi ili kuwahisha utekelezaji wa miradi iliyo kusudiwa.

Mkakati huo ulielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) Dr Maduhu Kazi wakati akikabidhi chuo cha ufundi stadi VETA kilichojengwa kwa msaada wa muwekezaji na kukabidhiwa kwa serikali.

Dr. Maduhu alisema kwamba ni wakati wa kuondoa upangufu uliokuwepo wa kuzania kwamba TIC ni kituo cha kupokea wawekezaji pekee, Badala yake wananchi washudue namna kituo hicho kinavyolea wawekezaji kwa akijili ya manufaa ya jamii.

Alisema, "Niwaombe wananchi waendelee kutoa ushirikiano ili maeneo ya uwekezaji yazidi kupatikana kwa wingi, kwani eneo linapokuwa na uwekezaji matokea yakebni kuongeza fursa za ajira pamoja na wigo wa kodi nchini,".

Awali aliongeza kuwa, uwekezaji unaofanywa hapa nchini ni kwa manufaa ya wananchi wenyewe kwa sababu inasaidia kuinua sekta ya kilimo ili mazao ya wakulima yaweze kuchakatwa na viwanda vya hapahapa nchini.

Hivyo malezi mazuri ya uwekezaji inakiwa ni  chachu ya maendeleo kwani wawekezaji wanapo nufaika wanainufaisha jamii kama ilivyokuwa kwa muwekezaji Alliance Ginneries kurudisha fadhira kwa jamii.

Ambapo katika amekabidhi shule moja ya msingi pamoja na chuo cha ufundi stadi kwa serikali akiwa na lengo la kusaidia wanajamii wa eneo ambalo amefanya uwekezaji.

Meneja mkuu wa kiwanda hicho Boaz Ogola alisema kuwa akiwa kama mwana jamii wa eneo hilo ni jukumu lake kuhakikisa anatatua changamoto mbali mbali za wanachi kwa sababu ndio wazalishaji wakubwa wa malighafi zinazo tumika katika kiwanda chake.

"Tunatekeleza maagizo ya serikali ya kuhakikisha tunashirikiana na jamii tunapo kuja kuwekeza ili kuhakikisha wananufaika na kuondoa changamoto ili waweze kuzalisha kwa ufanisi malighafi zinazo hitajika kiwandani," alisema Ogola.

Kiwanda hicho kimekabidhi vyumba vya madarasa vinane, jengo la utawala pamoja na matundu kumi ya vyoo, Yenye thamani ya shilingi milioni 150.

Mwisho.