@rosa_ree  amefanikiwa kujitengenezea nafasi yake muhimu kwenye game ya Hip Hop barani Afrika. Si ajabu tukisema kuwa kwa sasa ndio femcee tishio zaidi Afrika Mashariki. 


Lakini, kwa hapa nyumbani pia, thamani yake inazidi kuongezeka kila kukicha. Kuanzia kuwa moja ya wasanii wanaopiga show nyingi, hadi kuwa rapper wa kike anayetafutwa zaidi kwa collabo. 


Mwezi huu peke yake, ameshirikishwa kwenye ngoma mbili za wasanii wazito hapa Bongo. Alianza @bellachristian1 kwenye Only You, wimbo wa mapenzi ambao kwenye video yake yenye views zaidi ya 543k hadi sasa, wamejiachia utadhani wana uhusiano halisi. 


Wiki hii, legend @mrbluebyser1988 naye amemnasa Goddess kwenye Kibao Kata. Blue hajasita kumwamgia sifa kwa maneno mafupi lakini yenye uzito, “Goddess!!! Unajua sana KUCHANA.”

Kwa Nje ya nchi mwezi huu pekee ametokea katika Collabo mbili pia


Moja ikiwa Slovakia Aliyoshirikiswa katika Wimbo wa On Top wa Peter Pan, na nyingine Nchini Rwanda aliyoshirikishwa na Dj Pius katika Wimbo wa Tubushhe 



Pengine ni muda sahihi wa kumwahi mkali huyu kabla thamani yake haijawa maradufu, ikawa ngumu zaidi kumnasa!