Na Chelsea walikuwa tayari kumlipa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 33, mshahara wa £1m kwa wiki kwa uhamisho wenye thamani ya £225m mwaka 2014. (Sky Sports)

Juventus wanapanga uhamisho wa £360m kumnasa mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 21, klabu hiyo ya Serie A inaweza kumpeleka Cristiano Ronaldo upande wa pili. (Mirror)

Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund haina mpango wa kumuuza winga wa England Jadon Sancho, 21, katika dirisha dogo la usajili la January, ambaye alihusishwa na Manchester United katika majira ya joto. (Sport Bild, via Mail)

Cardiff City imekubali kumsajili winga wa Liverpool Harry Wilson kwa mkopo, huku vilabu vya Derby County na Nottingham Forest vikimwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider)

Arsenal inataka kuipiku Manchester United katika kumsajili mlinzi wa Villarreal, Pau Torres, 23, kwa kitita cha £35m mwezi January. (Express)

Middlesbrough inajaribu kukamilisha usajili wa winga Yannick Bolasie, 31, kwa mkopo kutoka Everton. (Sky Sports)

Klabu ya daraja la Kwanza England Swansea City inataka £18m kutoka Tottenham kwa ajili ya beki wake wa kati raia wa Wales Joe Rodon, 22. (Telegraph - subscription required)

Kuingo wa Manchester United Bruno Fernandes, 26, amekataa kumnyooshea kidole Ole Gunnar Solskjaer na wachezaji wenzake baada ya kipigo cha 6-1 kutoka kwa Tottenham kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa. (Sport TV, via Metro)

Mmiliki wa Derby County Mel Morris anasema meneja Phillip Cocu hatafukuzwa kama timu hiyo itafungwa ijumaa hii dhidi ya Watford, na kukataa pia taarifa kwamba mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney, 34, atambadili mdachi huyo.(Talksport)