Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, anataka kushinda taji la Uingereza msimu huu akiichezea Tottenham, kulingana na ajenti wake. (Sky Sports)

Arsenal inataka kuanzisha mazungmzo na Mesut Ozil kuhusu kufutilia mbali kandarasi yake kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Mail)

Manchester City imepiga hatua katika mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bryune .Wanataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutia saini kandarasi nyengine ya miaka 4. (Times)

Wachezaji wa soka wanaolipwa mapato ya juu zaidi duniani

Manchester United itajaribu kumsaini beki wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 21, kwa dau la £36.5m msimu ujao. Liverpool na Manchester City zina hamu ya kumsajili. (Bild, via Sun)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Memphis Depay, 26 anasema kwamba baadhi ya sheria zilimzuia kujiunga na Barcelona katika dirisha la uhamisho. (AS)

Aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea na Juventus Maurizio Sarri ni mgombea wa wadhfa wa meneja wa klabu ya Fiorentina. (Tuttomercato - in Italian)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Michael Cuisance, 21, amefutilia mbali madai kwamba kufeli kwa vipimo vya matibabu ndio sababu iliosababisha kufeli kwa uhamisho wakekujiunga na leeds . Baadaye alijiunga na Marseille , kwa mkopo kutoka Bayern Munich. (Sky Sports)

Liverpool itafanya mazungumzo na winga Harry Wilson kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mkopo katika klabu nyengine muda tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 atarudi baada ya mechi ya kimataifa akiichezea. (Standard)

Bournemouth haitamruhusu kiungo wa kati David Brooks kuondoka kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho. Sheffield United inamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 . (Football Insider)

West Ham inafikiria usajili wa £5m wa kiungo wa kati wa QPR na Ireland Ryan Manning. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto. (Star)

The Hammers pia wanataka kumsaini mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Josh King, 28, lakini wanaamini The Cherries inafaa kupunguza dau wanaloitisha la £17.. (Guardian)

Beki wa England Ashley Young, 35, anasema kwamba ataondoka Inter Miland na kuondoka Itali hivi sasa iwapo atarahusiwa kuichezea tena Watford.. (Golden Tales podcast)

Arsenal imeanza kuonesha moja kwa moja mechi zake kwa mashabiki wake katika ujwanja wa Emirates. Wataruhusu mashabiki 368