Tetemeko kubwa la ardhi limetokea Uturuki katika pwani ya Aegean n magharibi mwa fukwe ya Ugiriki ya Samos.

Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 7.0 lilipiga jimbo la Uturuki la Izmir , Watafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGS) wamesema kuwa lilisikika kwa mbali huko Athens na Istanbul.

Maofisa wa Uturuki wanasema hakuna ripoti ya waliojeruhiwa mpaka sasa lakini majengo sita yameanguka katika mji wa Izmir.

Uturuki na Ugiriki zinakabiliana na matetemeko ya ardhi mara kwa mara.

uturuki

Ripoti ya tetemeko la ardhi liliripotiwa fukwe ya Ugiriki ya Crete.

Video katika mitandao ya kijamii zinaonyesha jinsi watu wanavyotafuta wenzao katika majengo yaliyoanguka.

Walioshuhudia tukio hilo mjini Izmir walitawanyika katika mitaa mbalimbali wakati tetemeko hilo lilipopiga.

uturuki

Mwezi Januari mwaka huu, watu 30 waliuawa na wengine 1,600 walijeruhiwa na tetemeko lililopiga Uturuki katika jimbo la Elazig.

Julai mwaka jana, tetemeko lilipiga katika eneo kubwa la mji wa Athens huko Ugiriki.

Tetemeko lingine kubwa kupiga Uturuki lilipiga Izmit, karibu na Istanbul, mwaka 1999 na kuua watu 17,000.

The post Tetemeko kubwa latokea na kupiga Ugiriki na Uturuki appeared first on Bongo5.com.