Akiongea na shirika la habari la nchini Ufaransa, raisi wa kenya Uhuru Kenyatta amefunguka kwa mara ya kwanza baada jaji mkuu wa Kenya David Maraga kumsihi afanye hivyo kwa bunge kukeuka katiba kwa kutopitisha mswada wa sheria unaopendekeza kuwepo kwa usawa wa kijinsia.

“Sioni haja ya kulivunja bunge kwani hakuna uzito wowote kwenye pendekezo lililo letwa kwangu na jaji mkuu David Maraga.” Uhuru Kenyatta amekua nchini Ufaransa kwa ziara ya kidiplomsia, ikiwa ni safari yake ya kwanza nje ya nchi ya Kenya baada kufungua mipaka na shughuli za usafiri kurudi kama kawaida baada ya kifungwa duniani kote sababu kuu ikiwa kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa hatari wa Corona.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya

The post Sina mpango wakulivunja bunge! – Uhuru Kenyatta appeared first on Bongo5.com.