Jumba moja lenye uzito wa tani 7,600 lililazimishwa ‘kutembea’mjini Shanghai China. Jumba hilo lenye ghorofa tano la shule ya Lagena Elementary lililojengwa 1935 lilihamishwa ili kutoa nafasi kwa ujenzi mwengine karibu na eneo hilo.
Badala ya kulivunja jumba hilo la kihistoria , wahandisi waliamua kulienua na kuliweka katika miguu ya roboti kulingana na vyombo vya habari.
Maelfu ya tani ya jumba hilo yalihamishwa na kuwekwa umbali wa mita 61.7. katika mji huo wa mashariki mwa China.
Kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo CCTV , shughuli hiyo ilikamilishwa katika siku 18 na kukamilika mnamo tarehe 15 Octoba.
Hivi sasa jumba hilo linakarabatiwa kwa uhifadhi wa kihistoria
Kuna mbinu kadhaa za kuhamisha majengo , lakini wengi hutumia mbinu za kuhamisha kupitia reli au kreni.
lakini utumizi wa matairi ya roboti kama yale yanayotumika na shule ya Lagena ndio mbinu mpya inayotumiwa na wahandisi wa China.
Wachina wana wataalamu walio na uzoefu katika fani hii.
Mwaka 2017 , hekalu la dini ya Budha lililo na uzito wa tani 2000 lenye umri wa miaka 135 lilihamishwa umbali wa mita 30 ili kulizuia kuchomeka.
Baada ya siku 15 za kuhamishwa polepole, hatimaye jumba hilo la kihistoria liliwasili katika makao yake mapya. Mwaka huu , China iligonga vichwa vya habari kutokana na mradi mwengine wa miundo mbinu.
Ujenzi wa hopsitali ilioweza kubeba wagonjwa 1000 katika siku 10 pekee. Hospitali hiyo ilijengwa mjini Wuhan , Mji ambao mlipuko wa corona ulianzia.
https://bit.ly/2ToqOfz
The post Shuhudia jengo la shule lenye tani 7600 Shanghai linavyohamishwa (+Video) appeared first on Bongo5.com.