Beki wa kati wa timu ya taifa ya Ujerumani, Shkodran Mustafi, 28, amekataa ofa ya mkataba mpya Arsenal msimu wa majira ya joto na ameitaarifu klabu hiyo kwamba ana mipango ya kuondoka, wakati mkataba wake wa sasa utakapomalizika mwishoni mwa msimu (Football London)
Meneja wa Chelsea Frank Lampard yuko tayari kumjumuisha Antonio Rudiger kwenye mipango yake ya kikosi cha kwanza, kufuatia mazungumzo ya kina na mlinzi huyo wa kati wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 27, ambaye amekuwa akihusishwa na timu za Tottenham na Paris St-Germain. (Mail)
Crystal Palace imeanza mazungumzo na winga wa Uingereza Andros Townsend, 29, kuhusu mkataba mpya baada ya kufanikiwa kuzima mipango ya West Brom, iliyokua inamtaka majira ya joto (Football Insider)
Meneja wa West Brom Slaven Bilic amekasirishwa na mtendaji mkuu wa Baggies baada ya kumruhusu mlinzi wa Egypt Ahmed Hegazi, 29, kuondoka na kujiunga na Al-Ittihad inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia, bila yeye kujua (Sun)
Tottenham wanamatumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa mlinzi wa kushoto raia wa Uingereza Danny Rose, lakini nyota huyo mwenye miaka 30 anatarajia kutaka kulipwa zaidi ya £2.5m ya thamani ya mkataba wake uliobakia, ambao unakwisha June mwakani. (Football Insider)
Bodi ya ligi kuu England itaiweka kando katika juhudi zake za kuishawishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kuleta visa maalumu, baada ya Engalnd kujiondoa rasmi Umoja wa Ulaya. (Mail)
Watendaji wa ligi kuu hiyo watajadili na kubadili uamuzi kuhusu mfumo wa malipo ya kuangalia mechi baada ya watu wachache sana kujitokeza kulipia. (Mirror)
The post Shkodran Mustafi aichomolea Arsenal appeared first on Bongo5.com.