Watu watano wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kufanya fujo, kujeruhi na kusabababisha uharibifu wa mali,wakati msafara wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na chama cha Mapinduzi (CCM) walipokutana njiani wakitoka kwenye mikutano ya kampeni.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba

Vurugu hizo zilitokea jana majira ya saa moja jioni wakati msafara wa mgombea ubunge wa CCM Patrobas Katambi na mgombea ubunge wa CHADEMA Salome Makamba kukutana eneo la Japanise Corner nakuibua fujo ikiwemo kuharibu magari.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Ramadhan mohammed(20), Yuda Kanoku(22), Frank Chiza(20), Timoth Amos(20) na Mussa Luhende(21) wote wakiwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Pia Kamanda huyo amesema kuwa katika vurugu hizo Hasani Masanja(28) mkazi wa Mtaa wa Majengo alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kidevuni huku gari ya matangazo ya mgombea ubunge CCM lilivunjwa vioo vyote na magari mengine mawili yaliharibiwa pamoja

Aidha kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wanasiasa pamoja na wafuasi wao kuacha kufanya maandamano baada ya mikutano ya kampeni.

The post Shinyanga: Watu watano wakamatwa kwa kufanya fujo kwenye msafara wa CHADEMA na CCM ilipokutana njiani appeared first on Bongo5.com.