Serikali ya Sudan na makundi ya waasi jana imetia saini mkataba wa kihsitoria wa amani unaolenga kumaliza miongo kadhaa ya vita vilivyohujumu maisha ya mamia kwa maelfu ya watu.

Sudan, rebel groups sign historic peace deal | Deccan Herald

Kulikuwa na shamra shamra wakati wawakilishi wa serikali na makundi ya waasi walipotia saini hati ya mkataba huo kiasi mwaka mmoja tangu kuanza kwa mazunguzo ya kusaka amani.

Hafla ya kutia saini imehudhuriwa na wawakilishi wa Chad, Qatar, Mirsi, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

Mkataba huo unajumuisha masuala kadhaa yaliyo tete ikiwemo umiliki ardhi, mgawanyo wa madaraka na mapato ya serikali na kurejea kwa wakimbizi na raia waliopoteza makaazi wakati wote wa mzozo.

Kadhalika, chini ya hati hiyo ya makubaliano, wapiganaji wa makundi ya waasi kutoka majimbo ya Darfur, Kordofan ya Kusini na Blue Nile watajumuishwa kwenye vikosi vya jeshi la serikali.

The post Serikali, waasi wakubaliana amani Sudan appeared first on Bongo5.com.