Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati akifungua kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini,  Tirso Dos Santos akizungumza wakati wa kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkazi wa KOICA nchini Tanzania, Kyucheol Eo akitoa salamu za KOICA wakati wa kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN)  Hodan Addou akizungumza wakati wa kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu,  Joseph Rwiza akichangia maoni wakati wa kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri wa balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Viola Kuhaisa akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati inayosimamia mradi huo kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Tirso Dos Santos akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni washiriki wa kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo washiriki wa kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na mabinti wazazi kujitambua kupitia elimu nchini kilichofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kwamba itaendelea kushirikiana na mashirika ya kimataifa kuhakikisha kwamba kunakuwapo na maendeleo yenye uwiano wa kijinsia kwa kusaidia jamii kulielewa kundi la wasichana wasiokuwapo na wale walioacha shule kwa sababu mbalimbali na kulisaidia kundi hilo.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo wakati akiendesha kikao cha kamati inayosimamia mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri wa balehe na mabinti wazazi kujitambua na kushiriki katika kazi za uzalishaji mali.

Mradi huo ulianza mwaka 2016 na kutarajiwa kukamilika 2021 wenye thamani ya dola za Marekani milioni 5  unatarajiwa kunufaisha moja kwa moja watu 6000 na kunufaisha watu wengine milioni 2.5. Miongoni mwa wanufaika ni waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya na jamii ya wananchi.

Alisema mradi huo unaotekelezwa katika wilaya nne, kwenye mikoa minne ya Arusha (Ngorongoro), Kigoma (Kasulu), Mwanza (Sengerema) na Pemba (Mkoani) umelenga kuondoa vikwazo vyote vinavyowakabili mabinti wanaosoma na wale ambao hawasomi lakini wapo nyumbani.

Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UNWomen), Shirika la Idadi ya Watu Duniani  (UNFPA) na Shirika la Misaada ya Kimataifa la Korea Kusini (KOICA) na kuendeshwa chini ya uratibu wa Kamati ya Kitaifa ambapo serikali ndio mwenyekiti wake.

Katibu Kkuu Akwilapo alisema chini ya uratibu wa wizara yake, watu wengi wamefikiwa na kubadilisha maisha yao ikiwamo ya kufundisha walimu kutambua na kusaidia kuondoa vikwazo vinavyochochea ukatili dhidi ya mabinti kwa sababu za kiutamaduni, ndoa za mapema, mazingira yasiyorafiki kwa wanawake kusoma na upungufu katika utoaji wa elimu ya afya ya uzazi shuleni.

Vikwazo vingine ambavyo mradi umefunza walimu kutambua na kuviondoa ni mdondoko mkubwa wa wanafunzi, kushindwa mambo ya mpito kuelekea sekondari kutoka shule ya msingi na ukosefu wa utaalamu wa kuweza kuishi vyema na kuwa na kazi bora.

 Alisema katika mradi huo asilimia 65 ya miuondombinu iliyokusudiwa ya miradi kwa shule za msingi nI 85 kwa sekondari umetekelezwa na kusaidia kupunguza msuguano na ukatili dhidi ya mabinti.

Aidha mpaka mwaka huu mradi umetoa wanawake machampioni 208 kutoka katika wilaya hizo 4 ambao kazi yao ni kuhamasisha na kufunza wengine umuhimu wa kukabili vurugu katika shule na hivyo kusaidia elimu bora na salama kwa wasichana.

Pia kumetolewa visaidizi vya kuwawezesha wasichana kujua kusoma , kuandika na kuhesabu hata kwa kutumia vishakwambi katika vituo vilivyoteuliwa kutoa mafunzo hayo.

Katika mkutano huo wawakilishi kutoka mashirika yanayofadhili walisema kwamba wataendelea kuunga mkono mradi huo kutokana na umuhimu wake katika malengo mbalimbali ya dunia na hasa ya kuleta usawa wa kijinisa na maendeleo ya jamii kwa kubadili tamaduni na kuheshimu wanawake na mabinti na kuwapatia nafasi ya kukua kwa salama na kujipatia elimu sawa na wavulana.

Imeelezwa kwa sasa asilimia 53 tu ya wasichana wanaendelea na masomo ya sekondari kutoka elimu ya msingi wakati wavulana ni asilimia 58.

Katika mkutano washiriki walikubaliana kuimarisha matokeo chanya ya mradi huo na kuboresha elimu ya maarifa ya maisha kwa mabinti na kuwatengenezea mazingira salama ya kusoma na wale ambao hawajasoma wanawezeshwa kusoma kwa kuangalia pia mitaala iliyopo.