Msanii wa HipHop Roma Mkatoliki ametimiza miaka mitano ya ndoa yake na mkewe Mrs Roma, ambapo wamesheherekea kwa kutumiana ujumbe wa kupongezana na kutakiana kheri kwa walipo na wanapoelekea.

Msanii Roma na mkewe Mrs Roma siku ya harusi yao

Kupitia ukurasa wa Instagram anaoutumia Roma Mkatoliki, ametoa historia fupi kuhusu mahusiano yao yalipoanzia ambapo ameeleza kuwa “Nakumbuka kipindi kile miaka zaidi ya 11 iliyopita, ulivyokuwa unanitongoza nakukatalia, ukanitongoza mara ya pili nikakuchomolea ukawa unalia sanaa daaaah, mara ya tatu nikaja kukuonea huruma nikakukubalia tukaanza mahusiano, leo tuna miaka mitano kwenye ndoa yetu hakika Yehova ni mwaminifu

Huku kila nikitaka kuku-cheat inanijia ile sura yako ukilia mbele ya waandishi wa habari kipindi nimetekwa, ikinijia tu basi hisia zote zinakata naishiwa nguvu nawafukuzia mbali wazungu, navuta shuka nalala peke yangu, Mungu aendelee kudumisha ndoa yetu usiache kuniombea Shetani asije akanihadaa nami nafanya hivyo pia” ameongeza

Kwenye ndoa wamebarikiwa kupata watoto wawili ambao ni Ivan na Ivy, na kwa sasa msanii huyo wa HipHop yupo nchini Marekani tangu alivyoondoka Tanzania mwishoni mwa mwaka 2019.

View this post on Instagram

—————————————————————————————————————————————————–Msanii wa HipHop Roma Mkatoliki ametimiza miaka mitano ya ndoa yake na mkewe Mrs Roma, ambapo wamesheherekea kwa kutumiana ujumbe wa kupongezana na kutakiana kheri kwa walipo na wanapoelekea. Msanii Roma na mkewe Mrs Roma siku ya harusi yao Kupitia ukurasa wa Instagram anaoutumia Roma Mkatoliki, ametoa historia fupi kuhusu mahusiano yao yalipoanzia ambapo ameeleza kuwa "Nakumbuka kipindi kile miaka zaidi ya 11 iliyopita, ulivyokuwa unanitongoza nakukatalia, ukanitongoza mara ya pili nikakuchomolea ukawa unalia sanaa daaaah, mara ya tatu nikaja kukuonea huruma nikakukubalia tukaanza mahusiano, leo tuna miaka mitano kwenye ndoa yetu hakika Yehova ni mwaminifu" "Huku kila nikitaka kuku-cheat inanijia ile sura yako ukilia mbele ya waandishi wa habari kipindi nimetekwa, ikinijia tu basi hisia zote zinakata naishiwa nguvu nawafukuzia mbali wazungu, navuta shuka nalala peke yangu, Mungu aendelee kudumisha ndoa yetu usiache kuniombea Shetani asije akanihadaa nami nafanya hivyo pia" ameongeza  Kwenye ndoa wamebarikiwa kupata watoto wawili ambao ni Ivan na Ivy, na kwa sasa msanii huyo wa HipHop yupo nchini Marekani tangu alivyoondoka Tanzania mwishoni mwa mwaka 2019. ( Vi ROMA MKATOLIKI) Written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Roma amuandikia ujumbe mke wake: Huku nikitaka ku cheat inanijia sura yako unaliaa mbele ya waandishi wa habari (+Video) appeared first on Bongo5.com.