Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge amefanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es salaam kufuatilia kinachokwamisha kutoka kwa kontena zenye Vifaa vya ujenzi wa Stendi ya kisasa Mbezi Louis ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alietaka ujenzi wa Stendi hiyo kukamilika kabla ya Novemba 30 mwaka huu.

Katika ziara hiyo RC Kunenge amebaini udhaifu wa kiutendaji wa wakala kutoka kampuni ya Amazon General supply service na ushirikiano usiojitosheleza miongoni mwa Taasisi za umma zinazohusika kwenye mchakato mzima wa utoaji wa Mizigo bandarini.

Kutokana na hali hiyo RC Kunenge ametoa masaa mawili kwa Taasisi ya TICTS kuhakikisha kontena zilizokwama zinatoka na kuwaagiza TRA kuichunguza upya kampuni ya Amazon Kama inakidhi sifa na uwe wa kufanya kazi ya uwakala.

Aidha RC Kunenge amezielekeza taasisi za umma kuwa na ushirikiano Katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Serikali inayolenga kutatua kero za wananchi pamoja na wateja wengine wanaotumia Bandari ya Dar es salama.

Kwa mujibu wa RC Kunenge hadi siku ya leo mchana jumla ya kontena saba kati ya 13 za awali tayari zilikuwa zimeshatoka bandarini na kontena Sita ndio zinaanza kutoka leo huku kontena nyingine zikitarajiwa kutoka siku za karibuni.

The post RC Kunenge alivyofanya ziara ya kushtukiza bandarini, atoa masaa mawili kontena zilizozuiliwa kutoka mara moja (+Video) appeared first on Bongo5.com.