LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo Oktoba 19 kwa timu nne kushuka uwanjani kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Ratiba ipo namna hii:-

JKT Tanzania iliyo nafasi ya 16 na pointi nne itamenyana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 12 na pointi 5, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 8:00 mchana.

Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 13 na pointi tano itamenyana na Namungo FC iliyo nafasi ya nane na pointi tisa, saa 10:00 jioni.

Coastal Union iliyo nafasi ya 14 na pointi tano itamenyana na Biashara United iliyo nafasi ya nne na pointi 13, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.Saa 10:00 jioni.

Polisi Tanzania iliyo nafasi ya saba na pointi 10 itamenyana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 10 na pointi 7, saa 10:00 jioni.