Trump na mke wake wamepatikana na virusi vya corona baada ya kuwa kwenye karantini.

Coronavirus: Trump tests positive for Covid-19 with Melania Trump

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.

Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.

Tangazo hilo linawadia baada ya Bwana Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.

Bi. Hicks alisafiri na yeye kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii.

Baadae Alhamisi, Bwana Trump alisema yeye na mke wake wanakwenda karantini baada ya Bi. Hicks kuthibitishwa kuwa na corona.

Ameandika kwenye mtandao wa Twitter: “Hope Hicks, ambaye amekuwa akifanyakazi kwa bidii sana bila hata kupumzika, amethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19.

“Mke wangu na mimi tunasubiri matokeo yetu. Wakati huohuo, tutaanza mchakato wa kuwa kwenye karantini!”

Bado haijafahamika vile kuthibitishwa kwa Bwana Trump kutaathiri maandalizi ya mdahalo wa pili wa urais, ambao umepagwa kufanyika Oktoba 15 huko Miami, Florida.

The post Rais wa Marekani Donald Trump na mke wake wakutwa na CORONA appeared first on Bongo5.com.