Rais     Magufuli, amempigia simu mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma mjini, Zitto Kabwe, kwa lengo la kumjulia hali na kumtakia heri ili apone haraka baada ya hapo jana kupata ajali ya gari na kupata majeraha kadhaa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 7, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amempigia simu na kumpa pole Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, aliyepata ajali ya gari jana mkoani Kigoma, amemuombea heri ili apone haraka na pia amewashukuru madaktari na wauguzi wa kituo cha afya cha Kalya na Hospitali ya Maweni kwa matibabu waliyompa”, ameandika Msigwa.