Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya TUJUZANE

Android ===> GooglePlay


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia CHADEMA, Halima Mdee amehojiwa na Polisi kwa tuhuma za kumiliki vifaa vya kunasa sauti kinyume na Sheria za Mamlaka za Mawasiliano (TCRA)

 

Imeelezwa kuwa, jana Mdee alienda Kituoni kuripoti tukio la watu kumfuatilia na alipofika aliwekwa chini ya ulinzi akiambiwa kuna Jalada lake na anahitaji kufanyiwa upekuzi nyumbani

Upekuzi huo ulichukua zaidi ya saa moja na Jeshi la Polisi liliondoka nyumbani kwa Mgombea na kompyuta moja. Mdee aliachiwa kwa dhamana usiku baada ya kuchukuliwa maelezo