Kamishna wa Polisi Kaskazini Pemba Juma Saidi Hamisi, amesema Jeshi la Polisi humo limelazimika kutumia mabomu ya machozi usiku wa kuamkia leo Oktoba 27, 2020 ili kuwatawanya wananchi waliojitokeza kutaka kupiga kura.
Picha ya mfano (sio halisi kutoka kwenye tukio Polisi Kaskazini Pemba)
Kamishna Juma Saidi Hamisi, amesema wamefanya hivyo ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamejitokeza katika vituo vya kupiga kura za awali wakijiandaa kushiriki katika zoezi hilo licha ya kutokuwa sehemu ya kundi linalo husika na zoezi hilo.
Leo makundi mbalimbali visiwani Zanzibar yanapiga kura kuchagua viongozi huku wananchi wengine watafanya hivyo siku ya kesho Jumatano Oktoba 28, 2020.
The post Polisi Kaskazini Pemba watawanya wananchi appeared first on Bongo5.com.