Maafisa wakuu wa klabu ya Manchester United wamewasiliana na aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino iwapo watamfuta meneja Ole Gunnar Solskjaer. (Star)

Manchester City imekataa ofa ya dau la £15.4m na marupurupu kutoka kwa klabu ya Barcelona kumnunua beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.. (Sky Sports)

Liverpool ilipokea maombi ya winga wa Switzerland Xherdan Shaqiri, 28, wakati wa dirisha la uhamisho na wanataraji atasalia katika klabu hiyo hadi mwezi Januari kwasasabu hawako tayari kumuuza kwa mkopo (Goal)

Xhedan Shakiri

Beki wa Manchester City na England John Stones, 26, alikataa mbadala wa kuondoka kwa mkopo kuelekea Totenham kwasababu hakutaka kuiondoa familia yake. (Star)

Klabu ya Porto ina hamu ya kumnunua mchezaji wa West Ham na Brazil Felipe Anderson, 27, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Sky Sports)

West Ham iko katika mazungumzo ya kumsajili beki wa England mwenye umri wa miaka 30 Craig Dawson kutoka Watford. (Football Insider)

Barcelona imepoteza zaidi ya £181m kama mapato kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. (Telegraph)

Felipe Anderson

Mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel hafurahii hatua ya klabu hiyo kushindwa kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho. (Guardian)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

Matteo Guendouzi

Kiungo wa kati wa Arsenal Matteo Guendouzi, 21, anatarajiwa kuelekea katika timu ya ligi ya Bundesliga Hertha Berlin, baada ya kuwachwa nje ya kikosi cha timu hiyo katika uwanja wa Emirates. (Mirror)

Tottenham inatarajiwa kufanya jaribio la mwisho kumsaini beki wa InterMilan mwenye umri wa miaka 25 Slovakia defender Milan Skriniar. (Mirror)

Juventus inaandaa dau la kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea Emmerson Palmieri wakiwa na lengo la kumsaini mchezaji huyo wa Itali mwenye umri wa miaka 26 kwa. (Calciomercato – in Italian)

Arsenal imefutulia mbali mpango wao wa kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Ghana na Atletico Madrid Thomas Partey ,27. The Gunners haiko tayari kuafikia kifungu cha kumnunua mchezaji huyo cha £45m. (Mirror)

Thomas partey

Sheffield United inajiandaa kuipiku West Brom kumsajili mchezaji wa klabu ya Metz na Senegal mwenye umri wa miaka 25 Habib. (Le 10 Sport – in French)

Beki wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 20, huenda anaondoka Barcelona kwa mkopo, akitarajiwa kuelekea Fulham ambako anaelekea huku Everton pia nayo ikiwa ina hamu ya. (Le 10 Sport – in French)

Bayern Munich itamlenga winga wa Juventus na Brazil Douglas Costa, 30, iwapo watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 19. (Kicker – in German)

Celtic ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa West Ham Robert Snodgrass ,33 kwa mkopo lakini pia wako tayari kwa makubaliano ya kudumu.. (Sun)

Douglas Costa

Uhamisho wa beki wa Ujerumani Antonio Rudiger kuelekea AC Milan unaelekea kutimia , huku Chelsea ikifurahia kumwachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kabla ya mjadiliano ya kumuongozea kandarsi , huku akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake. (90min)

Anderlecht inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa West Ham na raia wa Ireland Josh Cullen, 24. (Het Laatste Nieuws – in Dutch)

Brighton inaandaa dau la 11.5m euro (£10.4m) kumnunua kiungo wa kati wa Poland Jakub Moder, 21, kabla ya kumuuza kwa mkopo kwa Lech Poznan kwa msimu huu. (Super Express – in Polish)

Kiungo wa kati wa klabu ya Valencia na jamhuri ya Afrika ya kati Geoffrey Kondogbia, 27, ananyatiwa na klabu isiojulikana kwa dau la 22m.(Marca – in Spanish)

Geoffrey Kondogbia,
Maelezo ya picha,Geoffrey Kondogbia,

Winga wa Roma na Uholanzi Justin Kluivert, 21, anaelekea RB Leipzig kwa mkopo wa muda mrefu (Fabrizio Romano via Football Italia)

Klabu ya Paris St-Germain imewasilisha ombi la kumnunua kwa mkopo beki wa Porto na Portugal Danilo Pereira, 29. (Goal)

Kiungo mshambuliaji wa Werder Bremen Davy Klaassen, 27, anatarajiwa kurudi katika klabu yake ya utotoni Ajax, baada ya dau la £10m kuafikiwa ili kumsajili mchezaji huyo wa Uholanzi. (De Telegraaf – in Dutch)

Mshambuliaji wa Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting, 31, atasaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Bayern Munich, baada ya kuondoka Paris St-Germain. (Kicker via Goal)

The post Ole Gunnar wa Man United aanza kukalia kuti kavu, mbadala wake apatikana appeared first on Bongo5.com.