Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama anafanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara leo mjini Phidadelphia kumpigia debe mgombea wa urais wa Marekani Joe Biden. 

Zikiwa zimebaki wiki mbili tu kabla ya uchaguzi huo, tofauti ya mikakati ya kampeni za wagombea hao ipo wazi. 


Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mwenye umri wa miaka 74, anaongoza mkutano mwingine wa kampeni katika jimbo muhimu la Pennsylvania, wakati mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden mwenye umri wa miaka 77, akibakia nyumbani Delaware ambako amejiweka karantini kabla ya mdahalo muhimu wa televisheni kati ya wagombea hao wawili kesho Alhamisi. 


Utafiti wa maoni unaonyesha kuwa Biden anaongoza dhidi ya Trump.