Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amemkosoa vikali Rais Donald Trump na serikali yake hapo jana juu ya namna alivyoshughulikia janga la ugonjwa wa COVID-19 nchini humo, wakati wa hotuba yake mbele ya wafuasi wa mgombea urais wa Democratic Joe Biden.
Obama amesema Trump hawezi kuwalinda Wamarekani, wakati anashindwa hata kuchukua hatua za msingi kujikinga yeye mwenyewe, akimaanisha kulazwa kwa rais huyo hospitalini wiki kadhaa zilizipita baada ya kuambukizwa virusi vya corona.
Kura za maoni ya umma zimeendelea kuonyesha kuwa Biden anaongoza kinyang’anyiro hicho cha urais dhidi ya Trump wa chama cha Republican. Aidha Obama amemkosoa Trump kwa kusema uwongo hadharani, pamoja na kushindwa kukemea tabia ya Wazungu kujipa hadhi ya juu nchini humo.
The post Obama amvaa Trump kuhusu Corona appeared first on Bongo5.com.