VITA NI VITA MURA! Msemo huo unaotumiwa na baadhi ya watu wa mkoa wa Mara kuchagiza ujasiri pindi kunapotokea hatari, unashabihiana na vita inayowakabili wasanii kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) baada ya kudaiwa kuiba mashairi na kuiga vipande vya video na kuviweka katika nyimbo zao mbili.


 


Wasanii hao ni Zuhura Kopa ‘ Zuchu’ pamoja na bosi wake Naseeb Abdul ‘ Diamond’ ambapo Septemba mwaka huu, waliachia ngoma mbili kwa mpigo, ambazo zinakimbiza kinoma katika mtandao wa YouTube na kuwaingizia mamilioni.


 


Nyimbo hizo ni ‘Cheche’ ambao uliachiwa Septemba 15, uliofi kisha watazamaji milioni 5.5 wakati ‘Litawachoma’ ulioachiwa Septemba 28 mwaka huu, umefi kisha watazamaji milioni 3.1, ilhali ule wa Alikiba- Mediocre ukifi kisha watamazaji milioni 2.3.


 


Hata hivyo, nyimbo hizo zimewajengea uhasama kwa baadhi ya mashabiki na wasanii kutoka nchi za Kenya na Marekani, kutokana na madai hayo ya kuiga style, kutumia mashairi bila idhini ya wamiliki halisi.


 


Licha ya kwamba nyimbo hizo mbili, Litawachoma na Cheche kuwa na mafanikio yaliyoweka rekodi ya kipekee, zimezidi kuwekewa pingamizi kwa njia mbalimbali, baada ya kutuhumiwa kuwa wasanii hao wametumia mistari ya Tanasha Dona (Kenya) na kuiga vipande vya staili kwenye video za wasanii Tobe Nwigwe na Beyonce Knowles kutoka Marekani.


 


SEPTEMBA 16


TANASHA DONNA


Siku moja baada ya Zuchu kuachia wimbo wa Cheche, mzazi mwenzake Diamond, Tanasha Donna mwenye makazi yake nchini Kenya, aliibuka na kudai baadhi ya mistari ya wimbo huo, imeibwa kutoka kwenye wimbo wake wa Ride aliomshirikisha Khagraph Jones.


 


Mistari ya Tanasha ya YO te quiero Tantee” ndiyo mistari sawa aliyotumia Zuchu kwenye intro ya wimbo wake wa Cheche. Kutokana na hilo, mashabiki wa Tanasha walimtupia vijembe Zuchu kutokana na madai ya kuiba mistari hiyo yenye lugha ya Kispanyiola.


 


Aidha, Meneja wake Tanasha; Jamal Gaddaffi , naye aliwasuta Diamond na Zuchu kwa kudai kuwa, wanakosa ubunifu. Hata hivyo, Zuchu alisema katika maisha yake ndani ya sanaa hiyo, hajawahi kutumia muda wake wala kufi kiria kucopy kazi ya mtu mwingine.


 


“Mimi nimeumizwa sana na kauli hizo, kwangu si rahisi, natumia muda mwingi kuumiza akili kupata kitu kizuri nikaandika mashairi mwenyewe, kuna wakati nakosa hata muda wa kuingia kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuwa busy. Naomba nieleweke, sijawahi kucopy kazi ya mtu,” alisema Zuchu.


 


BEYONCE KNOWLES


Wakati tuhuma hizo zikiwa hazijapoa, video ya wimbo huo wa Cheche, pia ilidaiwa kuwa wameiga style kutoka kwenye wimbo wa Beyoncé unaofahamika kwa jina la Naughty Girl. Baadhi ya mashabiki walieleza kuchukizwa na hatua hiyo, kutokana na vipande vya video za nyimbo hizo mbili kufanana.


 


“Kutumia idea ya mtu mwingine sio dhambi, shida inakuja pale unapotumia bila ridhaa yake, ndipo mambo yanayowakuta wasanii wengine,” alisema Godfrey Newton. Aidha, hoja hiyo ya Newton, iliungwa mkono na shabiki mwingine ambaye aliandika katika mtandao wa Twitter kuwa “Hata wasanii wakubwa duniani, wanatumia idea za watu wengine, ila cha msingi ni kufuata utaratibu.”


 


RAPA TOBE NWIGWE


Katika kudhihirisha kuwa vita dhidi ya wasanii hao ni kubwa, Msanii mahiri wa muziki wa kufokafoka ‘Hiphop’ kutoka nchini Marekani, Rapper Tobe Nwigwe naye aliibuka na kudai kuwa Zuchu na Mondi wameiba style za vipande vya video yake katika wimbo wa ‘Eat’.


 


Picha lilianza kwa Mchekeshaji kutoka nchini humo, Kevon Stage ambaye alimtaka Diamond kuufuta wimbo huo wa Litawachoma, baada ya kudai kuwa walitumia idea ya rapa Tobe Nwigwe. Mchekeshaji huyo ambaye ni rafi ki wa karibu wa Tobe, alirekodi video akiwa anamchana Diamond na kumtaka kufuta vipande hivyo kwenye wimbo wake.


 


“Najua umeiba staili ya Tobe, nimeenda YouTube nimeona kweli umechukua staili zake katika mavazi ya kijani kibichi, huku akiwa amekaa na familia kwenye sofa, nyingine amevaa mavazi ya ngozi ya chui na yote umeiga, tafadhali nenda kafute,” alisema Kevon Stage.


 


Hata hivyo, Rapper Tobe kupitia mtandao wake wa Instagram, aliwapongeza Diamond na Zuchu kwa kile alichodai kuwa, wamevutiwa na kazi zake ambayo wanadaiwa kuiga. Hii si mara ya kwanza kwa wasanii kutoka label ya WCB, kudaiwa kuiga vipande vya video kutoka katika kazi za wasanii wengine.