Matukio mengi ambayo watu wameokolewa baada ya kufungwa kwa miaka mingi na familia zao kumewashtua Wanaigeria, na kuangazia yanayofanywa na wazazi na ukosefu wa utoaji wa huduma za afya ya akili.

Baadhi ni wakubwa, wanaoelezwa kuwa na ugonjwa wa akili, walikutwa wakiwa na minyororo ikiwa imezungushwa kwenye vifundo vya miguu yao, na wakishurutishwa kula, kulala na kujisaidia ndani ya eneo hilo hilo walimofungiwa.

Katika kisa cha mwanaume mmoja mwenye miaka 32, alifungwa kwa miaka saba kwenye gereji ya wazazi wake Kaskazini-Magharibi mwa jimbo la Kano.

Kulikuwa na ripoti za watoto kunyanyaswa wakiwa chini ya uangalizi wa mama wa kambo au walezi.

Katika tukio la karibuni mwezi Septemba, mama wa kambo wa mtoto wa miaka saba alikamatwa baada ya kudaiwa kumpiga hadi kifo nyumbani huko Kano, jimbo kubwa zaidi nchini Nigeria.

Mama wa kambo bado hajashtakiwa, na hajazungumza lolote.

Mvulana katika banda la kuku

Wakati kuna matukio ya unyanyasaji wa watoto kote Nigeria, eneo la kaskazini limekuwa likitazamwa zaidi hivi karibuni lililosababishwa na tukio la mwezi Agosti kuhusu mtoto wa miaka 11 ambaye alikuwa amefungiwa katika banda la kuku katika jimbo la Kebbi, wakati baba yake na mama wa kambo, ambao sasa wameshtakiwa mahakamani, waliishi kwa raha ndani ya nyumba.

Tukio hilo

Tukio hilo lilisababisha ghadhabu baada ya kuonekana picha ya mtoto huyo akiwa amechuchumaa kando ya kuku na bata mzinga

Baada ya kesi hiyo huko Kebbi, tulianza kupata taarifa, “alisema Haruna Ayagi, mkuu wa Mtandao wa Haki za Binadamu (HRN), shirika lisilo la kiserikali ambalo limehusika katika uokoaji wa watu 12, saba kati yao watoto, mwezi Agosti peke yake, katika jimbo la Kano.

”Tulichobaini ni kuwa watoto ambao walikuwa wakinyanyasika hawakuwa wakiishi na mama zao wa kuwazaa,” aliongeza Bwana Ayagi.

Katika mji mkuu Abuja, watoto wawili waliokolewa kutoka kwenye choo, ambapo inaaminika walikuwa wakifungiwa humo kila siku na mama yao wa kambo mpaka anaporejea kutoka kazini.

‘Kupigwa, kuchomwa moto na kuachwa na njaa’

Baadhi ya picha za watoto waliotendewa vibaya zilionekana kama picha kutoka kwa sinema ya Nollywood, ambapo tabia ya mama wa kambo mkatili imekuwa dhana ya watu wengi wa Nigeria wanayoijua, ingawa kuna mama wa kambo wengi ambao huwatunza vyema watoto ambao si wa kuwazaa.

Katika kisa kimoja huko Kano, msichana wa miaka saba alidaiwa kupigwa, kuchomwa moto na kuachwa na njaa na mama yake wa kambo, kulingana na taarifa za mamlaka.

Msichana huyo, na watoto wengine waliookolewa huko Kano, sasa wako katika nyumba ya serikali kutunza watoto , wakipokea matibabu na ushauri nasaha, wakati wazazi na walezi wengine wamekamatwa, lakini bado hawajashtakiwa.

Sheria ya mwaka 2003 inayolinda haki za watoto inaipa serikali haki ya kuchukua mtoto anayeshukiwa kuwa “amepuuzwa au kutendewa vibaya”.

Lakini majimbo 11 ya Kaskazini, likiwemo Kano, bado hayajapitisha sheria, kwasababu ya upinzani uliopo kuhusu kumtambua mtoto kuwa yeyote aliye chini ya miaka 18 na hivyo kuzuia ndoa za watoto zinazofanyika kwenye eneo hilo.Baadhi ya Waislamu wanaamini kuwa mvulana anapobalehe na msichana kuvunja ungo, maana yake si watoto na wanaweza kuoa au kuolewa.

Mzozo huu umekuwa ukizuia kupitishwa kwa sheria katika majimbo 11, na inakuwa vigumu kwa serikali kuingilia kati kesi za namna hiyo.

”Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto vimefanywa kama vya kawaida”, anasema Imaobong Ladipo Sanusi, Mku wa shirika la Wotclef, linalofanya kampeni ya kutetea haki za wanawake na watoto.

Unyanyapaa kwa kuwa mgonjwa wa akili

Kijana wa miaka 30 aliokolewa kutoka eneo la kuegesha magari nyumbabi kwa wazazi wake huko Kano, ambapo majirani walisema alikuwa amefungiwa kwa miaka saba kwa madai ya kuwa mgonjwa wa akili, hakuweza kutembea alipopatikana.

Miguu yake ilikuwa imepinda miguu ilikuwa dhaifu sana kuusaidia mwili wake uliokuwa umekonda sana.

Katika kisa kingine huko Kano, mwanamume wa miaka 55 alipatikana akiwa amejifungiwa ndani ya chumba kisicho na dirisha. Mguu wake mmoja ulikuwa umefungwa kwenye gogo kubwa lenye chuma.

Alikuwa amefungwa na familia yake kwa miaka 30 kwa sababu alikuwa mgonjwa wa akili, na alipelekwa Hospitali Kuu ya Rogo. Daktari katika hospitali hiyo, Luis Nweke, alithibitisha kuwa ana matatizo ya akili.

Kwa miaka mingi, Nigeria imekuwa ikijitahidi kuwatunza wagonjwa wa akili, kwa sababu ya unyanyapaa unaohusishwa na maradhi hayo.

Katika jamii nyingine, ugonjwa wa akili huonekana kama mwiko na wagonjwa wa akili hujulikana kama “watu wenye wazimu”, waliotengwa na familia zao, waliolazimika kuzurura barabarani wakiwa wamevaa nguo chakavu na kula majalalani.

“Kesi za kaskazini ni kielelezo cha kile kinachotokea Nigeria. Suala hili la kuwafungia wagonjwa wa akili na kuwatendea vibaya ni suala lililoenea kote nchini,” mkuu wa umoja wa madaktari wa akili, Dk Taiwo Lateef, aliambia BBC .

Takwimu za hivi karibuni kuhusu idadi ya watu wanaohitaji matibabu haipatikani, lakini kwa wataalam wa magonjwa ya akili chini ya 300 katika nchi yenye idadi ya watu karibu milioni 200, familia mara nyingi huelekea kwenye vituo vya uponyaji vya jadi, na vituo vya imani, zote ni za Kikristo. na Kiislamu.

“Kwa sababu watu wengi wanaona ugonjwa wa akili kama shida ya kiroho, wanatafuta msaada kutoka kwa viongozi wa kiroho na waganga wa jadi wanaotarajia kutoa roho mbaya inayohusika,” alisema Dk Oluseun Ogunnubi, mtaalamu wa magonjwa ya akili.

Ripoti ya 2013 na wizara ya afya ya Nigeria ilisema takribani 10% ya idadi ya watu wamepata matatizo ya akili. Chini ya 10% ya idadi hiyo walipata huduma wanayohitaji, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Ingawa ukosefu wa vituo vya afya ya akili ni sehemu ya changamoto kubwa ndani ya sekta ya afya, ukweli kwamba kuna vituo vya chini ya 15 vya serikali vinavyotoa huduma kwa wagonjwa ya akili kote nchini hufanya ufikiwaji wa huduma hii kwa watu wengi, hasa vijijini.

Lakini hata katika maeneo ambayo vituo vya huduma za afya ya akili vinapatikana,unyanyapaa unaohusishwa na kuchukua wapendwa wao kwa ajili ya matibabu huzuia familia nyingi kufanya hivyo.

“Watu wengi hawataki hata kuonekana wakiingia katika hospitali za magonjwa ya akili kwa sababu ya taarifa za uongo na imani potofu kuhusu afya ya akili,” alisema Dk Lateef.

“Watu wanaishi kwa kuikataa hali halisi kwa sababu ya unyanyapaa. Inawezaje kusema kuwa nina ugonjwa wa akili, kwa sababu hawajawahi kuukubali kama ni aina ya ugonjwa?” Aliuliza.

ghadhabu baada ya kuonekana picha ya mtoto huyo akiwa amechuchumaa kando ya kuku na bata mzinga

Mtoto akiwa amefungiwa kwenye banda la kuku

Baada ya kesi hiyo huko Kebbi, tulianza kupata taarifa, “alisema Haruna Ayagi, mkuu wa Mtandao wa Haki za Binadamu (HRN), shirika lisilo la kiserikali ambalo limehusika katika uokoaji wa watu 12, saba kati yao watoto, mwezi Agosti peke yake, katika jimbo la Kano.

”Tulichobaini ni kuwa watoto ambao walikuwa wakinyanyasika hawakuwa wakiishi na mama zao wa kuwazaa,” aliongeza Bwana Ayagi.

Katika mji mkuu Abuja, watoto wawili waliokolewa kutoka kwenye choo, ambapo inaaminika walikuwa wakifungiwa humo kila siku na mama yao wa kambo mpaka anaporejea kutoka kazini.

‘Kupigwa, kuchomwa moto na kuachwa na njaa’

Baadhi ya picha za watoto waliotendewa vibaya zilionekana kama picha kutoka kwa sinema ya Nollywood, ambapo tabia ya mama wa kambo mkatili imekuwa dhana ya watu wengi wa Nigeria wanayoijua, ingawa kuna mama wa kambo wengi ambao huwatunza vyema watoto ambao si wa kuwazaa.

Mtoto

Katika kisa kimoja huko Kano, msichana wa miaka saba alidaiwa kupigwa, kuchomwa moto na kuachwa na njaa na mama yake wa kambo, kulingana na taarifa za mamlaka.

Msichana huyo, na watoto wengine waliookolewa huko Kano, sasa wako katika nyumba ya serikali kutunza watoto , wakipokea matibabu na ushauri nasaha, wakati wazazi na walezi wengine wamekamatwa, lakini bado hawajashtakiwa.

Sheria ya mwaka 2003 inayolinda haki za watoto inaipa serikali haki ya kuchukua mtoto anayeshukiwa kuwa “amepuuzwa au kutendewa vibaya”.

Lakini majimbo 11 ya Kaskazini, likiwemo Kano, bado hayajapitisha sheria, kwasababu ya upinzani uliopo kuhusu kumtambua mtoto kuwa yeyote aliye chini ya miaka 18 na hivyo kuzuia ndoa za watoto zinazofanyika kwenye eneo hilo.Baadhi ya Waislamu wanaamini kuwa mvulana anapobalehe na msichana kuvunja ungo, maana yake si watoto na wanaweza kuoa au kuolewa.

Mzozo huu umekuwa ukizuia kupitishwa kwa sheria katika majimbo 11, na inakuwa vigumu kwa serikali kuingilia kati kesi za namna hiyo.

Watoto watatu wakifanya biashara

”Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto vimefanywa kama vya kawaida”, anasema Imaobong Ladipo Sanusi, Mku wa shirika la Wotclef, linalofanya kampeni ya kutetea haki za wanawake na watoto.

Unyanyapaa kwa kuwa mgonjwa wa akili

Kijana wa miaka 30 aliokolewa kutoka eneo la kuegesha magari nyumbabi kwa wazazi wake huko Kano, ambapo majirani walisema alikuwa amefungiwa kwa miaka saba kwa madai ya kuwa mgonjwa wa akili, hakuweza kutembea alipopatikana.

Waokoaji walilazimika kukata mnyororo ili kumwokoa mtu huko Kano

Miguu yake ilikuwa imepinda miguu ilikuwa dhaifu sana kuusaidia mwili wake uliokuwa umekonda sana.

Katika kisa kingine huko Kano, mwanamume wa miaka 55 alipatikana akiwa amejifungiwa ndani ya chumba kisicho na dirisha. Mguu wake mmoja ulikuwa umefungwa kwenye gogo kubwa lenye chuma.

Alikuwa amefungwa na familia yake kwa miaka 30 kwa sababu alikuwa mgonjwa wa akili, na alipelekwa Hospitali Kuu ya Rogo. Daktari katika hospitali hiyo, Luis Nweke, alithibitisha kuwa ana matatizo ya akili.

Kwa miaka mingi, Nigeria imekuwa ikijitahidi kuwatunza wagonjwa wa akili, kwa sababu ya unyanyapaa unaohusishwa na maradhi hayo.

Katika jamii nyingine, ugonjwa wa akili huonekana kama mwiko na wagonjwa wa akili hujulikana kama “watu wenye wazimu”, waliotengwa na familia zao, waliolazimika kuzurura barabarani wakiwa wamevaa nguo chakavu na kula majalalani.

Data za wataalamu wa magonjwa ya akili katika baadhi ya nchi

“Kesi za kaskazini ni kielelezo cha kile kinachotokea Nigeria. Suala hili la kuwafungia wagonjwa wa akili na kuwatendea vibaya ni suala lililoenea kote nchini,” mkuu wa umoja wa madaktari wa akili, Dk Taiwo Lateef, aliambia BBC .

Takwimu za hivi karibuni kuhusu idadi ya watu wanaohitaji matibabu haipatikani, lakini kwa wataalam wa magonjwa ya akili chini ya 300 katika nchi yenye idadi ya watu karibu milioni 200, familia mara nyingi huelekea kwenye vituo vya uponyaji vya jadi, na vituo vya imani, zote ni za Kikristo. na Kiislamu.

“Kwa sababu watu wengi wanaona ugonjwa wa akili kama shida ya kiroho, wanatafuta msaada kutoka kwa viongozi wa kiroho na waganga wa jadi wanaotarajia kutoa roho mbaya inayohusika,” alisema Dk Oluseun Ogunnubi, mtaalamu wa magonjwa ya akili.

Ripoti ya 2013 na wizara ya afya ya Nigeria ilisema takribani 10% ya idadi ya watu wamepata matatizo ya akili. Chini ya 10% ya idadi hiyo walipata huduma wanayohitaji, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

Ingawa ukosefu wa vituo vya afya ya akili ni sehemu ya changamoto kubwa ndani ya sekta ya afya, ukweli kwamba kuna vituo vya chini ya 15 vya serikali vinavyotoa huduma kwa wagonjwa ya akili kote nchini hufanya ufikiwaji wa huduma hii kwa watu wengi, hasa vijijini.

Lakini hata katika maeneo ambayo vituo vya huduma za afya ya akili vinapatikana,unyanyapaa unaohusishwa na kuchukua wapendwa wao kwa ajili ya matibabu huzuia familia nyingi kufanya hivyo.

“Watu wengi hawataki hata kuonekana wakiingia katika hospitali za magonjwa ya akili kwa sababu ya taarifa za uongo na imani potofu kuhusu afya ya akili,” alisema Dk Lateef.

“Watu wanaishi kwa kuikataa hali halisi kwa sababu ya unyanyapaa. Inawezaje kusema kuwa nina ugonjwa wa akili, kwa sababu hawajawahi kuukubali kama ni aina ya ugonjwa?” Aliuliza.

View this post on Instagram

————————————————————————————–Matukio mengi ambayo watu wameokolewa baada ya kufungwa kwa miaka mingi na familia zao kumewashtua Wanaigeria, na kuangazia yanayofanywa na wazazi na ukosefu wa utoaji wa huduma za afya ya akili. Baadhi ni wakubwa, wanaoelezwa kuwa na ugonjwa wa akili, walikutwa wakiwa na minyororo ikiwa imezungushwa kwenye vifundo vya miguu yao, na wakishurutishwa kula, kulala na kujisaidia ndani ya eneo hilo hilo walimofungiwa. Katika kisa cha mwanaume mmoja mwenye miaka 32, alifungwa kwa miaka saba kwenye gereji ya wazazi wake Kaskazini-Magharibi mwa jimbo la Kano. Kulikuwa na ripoti za watoto kunyanyaswa wakiwa chini ya uangalizi wa mama wa kambo au walezi. Katika tukio la karibuni mwezi Septemba, mama wa kambo wa mtoto wa miaka saba alikamatwa baada ya kudaiwa kumpiga hadi kifo nyumbani huko Kano, jimbo kubwa zaidi nchini Nigeria. Mama wa kambo bado hajashtakiwa, na hajazungumza lolote. Mvulana katika banda la kuku Wakati kuna matukio ya unyanyasaji wa watoto kote Nigeria, eneo la kaskazini limekuwa likitazamwa zaidi hivi karibuni lililosababishwa na tukio la mwezi Agosti kuhusu mtoto wa miaka 11 ambaye alikuwa amefungiwa katika banda la kuku katika jimbo la Kebbi, wakati baba yake na mama wa kambo, ambao sasa wameshtakiwa mahakamani, waliishi kwa raha ndani ya nyumba. Tukio hilo lilisababisha ghadhabu baada ya kuonekana picha ya mtoto huyo akiwa amechuchumaa kando ya kuku na bata mzinga Mtoto akiwa amefungiwa kwenye banda la kuku Baada ya kesi hiyo huko Kebbi, tulianza kupata taarifa, "alisema Haruna Ayagi, mkuu wa Mtandao wa Haki za Binadamu (HRN), shirika lisilo la kiserikali ambalo limehusika katika uokoaji wa watu 12, saba kati yao watoto, mwezi Agosti peke yake, katika jimbo la Kano. ''Tulichobaini ni kuwa watoto ambao walikuwa wakinyanyasika hawakuwa wakiishi na mama zao wa kuwazaa,'' aliongeza Bwana Ayagi. Katika mji mkuu Abuja, watoto wawili waliokolewa kutoka kwenye choo, ambapo inaaminika walikuwa wakifungiwa humo kila siku na mama yao wa kambo mpaka anaporejea kutoka kazini. 'Kupigwa, kuchomwa moto na kuachwa na njaa' ( Via Human Rights Watch) Written by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

The post Nigeria: Yabainika wagonjwa wa akili hufungiwa ndani kwa kufungwa minyororo (+Video) appeared first on Bongo5.com.